
BIBI AJIELEZA, AJICHANGANYA
Bibi huyo, akiwa amezingirwa na umati wa wananchi wenye hasira kali,
alipotakiwa ajieleze alikotokea, alijichanganya kwani jibu lake la
kwanza alidai ameanguka kutoka angani akitokea Tabora.
Alipozidi kubanwa kwa maswali, alibadili kauli na kusema alianguka akiwa
safarini kutokea Tanga, kauli zilizowapandisha hasira wananchi wenye
imani potofu za ushirikina, wakiongozwa na dada mmoja aliyejitangaza
kuwa amepandisha mashetani na kudai eti bibi huyo ni mwanga kwa mujibu
wa mashetani yake.
MASHETANI YACHOCHEA HASIRA
Mashetani ya dada huyo yalizidi kuwaongeza hasira wananchi hao wenye
imani za kishirikina ambao walianza kukusanya vitambaa na makaratasi ya
maboksi huku wengine wakianza kutafuta mafuta ya taa ili wamwagie kisha
wamchome moto bibi kizee huyo, ndipo walipotokea wasamaria wema
waliomuokoa na Kumpelea polisi.
POLISI WANENA
Kufuatia tukio hilo, siku iliyofuata mwanahabari wetu alifika kituo cha
polisi alichokimbizwa bibi huyo ili kupata ukweli zaidi ambapo askari
mmoja aliyekutwa kituoni hapo, aliyeomba jina lake lisiandikwe kwenye
mitandao kwa kuwa siyo msemaji wa jeshi hilo, alikiri kupokelewa kwa
kikongwe huyo.
“Ni kweli bibi huyo aliletwa hapa kituoni saa tisa usiku lakini kulikuwa
hakuna kosa lolote la jinai tuliloona kuwa anastahili kufunguliwa
mashitaka. Jeshi la polisi haliamini ushirikina, baada ya watu
kutawanyika na kuona kuna usalama tulimuachia, tumefarijika kuona
wananchi hawakujichukulia sheria mikononi, waendelee kufanya hivyo.”
alisema askari huyo
CHANZO: DJ SEK BLOG





No comments:
Post a Comment