MZEE KIPARA

Mwanzoni mwa mwezi Januari, mwigizaji wa siku nyingi Bongo, Said Fundi ‘Mzee Kipara’ alifariki dunia akiwa kwenye nyumba ya Kundi la Sanaa la Kaole, Kigogo jijini Dar baada ya kusumbuliwa na maradhi mbalimbali yaliyomuandama kwa muda mrefu na utu uzima.
KANUMBA

Kanumba alifariki alfajiri ya Jumamosi Aprili 7, akiwa na umri wa miaka 28, baada ya kile kilichodaiwa kuwa ugomvi wa kimapenzi na rafiki yake wa kike, ambaye pia ni mwigizaji, anayefahamika kwa jina Elizabeth Michael, maarufu ‘Lulu’.
Umati wa watu wakiwamo Rais Jakaya Kikwete,
maoafisa waandamizi wa Serikali, wasanii na watu wa tabaka mbambali
walihudhuria msiba huo, ambapo pia walikusanyika katika viwanja vya
Leader’s kutoa heshima zao za mwisho kabla ya mazishi yaliyofanyika
makaburi ya Kinondoni.
Idadi hiyo kubwa inayoingia katika rekodi za pekee
ni ya pili kutokea baada ya umati uliofurika wakati wa kuaga mwili wa
Baba wa Taifa, Mwalimu Julias Kambarage Nyerere.
Huo ni ushahidi tosha wa umaarufu mkubwa aliokuwa nao Kanumba, ambaye hadi mauti yalipomkuta aliweza kutengeneza zaidi ya filamu 40 akishirikiana na wasanii mbali mbali ndani na nje ya nchi na hasa Nigeria.

MAFISANGO
Alikuwa mchezaji wa klabu ya Simba ya Jijini Dar es Salaam, aliyezaliwa Machi tisa mwaka 1980 na kufariki Mei 17 mwaka 2012 kwa ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Tanzara, alipokuwa akijaribu kumkwepa mwendesha pikipiki, ambapo gari lake lilipoteza mwelekeo, kuacha njia na kutumbukia mtaroni na kugharimu maisha ya mchezaji huyo, ambaye pengo lake hadi sasa Simba wameshindwa kuliziba.
Mafisango aliagwa kwenye viwanja vya Chang'ombe na kwenda kuzikwa kwenye Kijiji cha Lembe Kinshansa nchini Kongo.
Kifo chake kiliacha taaruki kubwa hasa kwa wapenzi
wa soka kwani alikuwa ni mchezaji wa aina yake Simba, hakuwahi kuwa
nahodha wa timu kama kwenye timu yake ya APR ya Rwanda na Amavubi,
lakini alikuwa ni zaidi ya nahodha kwani aliweza kuhamasisha wenzake
kucheza bila kuchoka na kutokata tamaa hata pale Simba inaposhambuliwa
na timu pinzani na au hata kufungwa.
MARIAM KHAMIS

Mwezi Novemba kilio kilisikika kwenye muziki wa Taarab baada ya kufariki ghafla kwa staa wa Kundi la Tanzania One Theater (TOT), Mariam Khamis ‘Paka Mapepe’ alipokuwa akijifungua.
MLOPELO

Pia Novemba mwaka huu, mwigizaji aliyepata umaarufu mkubwa enzi za Kaole Sanaa Group kupitia runinga ya ITV, Khalid Mohamed ‘Mlopelo’ alifariki dunia kwenye Hospitali ya Temeke, Dar baada ya kuwa na maumivu ya mwili kwa muda mrefu.
JOHN MAGANGA
.Aliyekua muigizaji wa tasnia ya Bongo Movie marehemu, John Stephan Maganga ambaye filamu yake ya mwisho inayoweza kuwakumbusha watu wengi taswira yake, kwa wale wanaotaka kumjua ni “BAR AHMED” iliywashirikisha Nice na Irene Uwoya, ambapo Marehemu Stephano ali act kama Boss wa bar ambaye alimwambukiza gonjwa la ukimwi Irene Uwoya.
Baba yake mdogo na marehemu, ambaye pia naye ni mwigizaji, alielezea mkasa mzima toka Stephan alipoanza kuumwa mpaka siku ya kifo chake jumamosi asubuhi baada ya kuugua kwa muda mfupi na kulazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar
Baba mdogo wa Stephano anasema, kabla ya kufikwa na umauti mwigizaji John alikuwa akisumbuliwa na homa ambapo alimpigia simu na kumweleza jinsi anavyojisikia ndipo akamwambia amngojee, kisha alimfuata na kumpeleka Hospitali ya Mwananyamala
SHARO MILIONEA
Mwenzi huohuo wa gundu, mwigizaji na mwanamuziki, Hussein Ramadhan Mkieti ‘Sharo Milionea’, alifariki dunia kutokana na ajali ya gari iliyotokea usiku katika eneo la Maguzoni Songa katikati ya Segera na Muheza mkoani Tanga alipokuwa safarini kuelekea nyumbani kwao Muheza kumpelekea mama yake fedha za matumizi.Namna ya uigizaji wake katika hali ya kitanashati na mikogo ya kipekee inayoendana na lugha ya ‘kisharobaro’, ilimfanya msanii huyo kupoteza jina lake halisi ambalo ni Husseni Ramadhani Mkieti.
Ilikuwa vigumu kumsaka msanii huyo kwa jina lake halisi, lakini ilikuwa ni rahisi kumpata iwapo ungemtafuta kwa jina la Sharo Milionea.
Msani huyo alibadilisha jina lake la awali na
Sharobaro na kuwa Sharo Milionea, baada ya kuingia mzozo na msanii
mwenzake, Bob Junior ambapo kwa kuepusha wasikosane, aliamua kutumia
jina hilo jipya lililokolea na kumvaa kuliko maelezo.
Katika mahojiano mbali mbali Sharo Milionea
aliwahi kunukuliwa akisema kuwa alipenda kuigiza kama brazameni akitumia
maneno kama 'usinichafue meen', 'nimechoka kuimba meen' kamata 'mwizi
meen' ili kujitofautisha na wasanii wengine nchini, akiiga staili ya
msanii aliyekuwa akimhusudu, Will Smith.
Sharo Milionea, aliyekuwa mahiri kwa kuigiza
filamu na uimbaji wa muziki wa kizazi kipya, alikiri kwamba karibu kila
jambo katika sanaa yake, ina chembe ya nyota huyo wa Kimarekani
anayetamba kwenye muziki na filamu ulimwenguni.
Mkali huyo aliyewahi kutamba na nyimbo kama
'Nahesabu Namba','Tusigombane', 'Chuki Bure', 'Hawataki', 'Sondela',
'Tembea Kisharobaro' ambaye pia alikuwa mbioni kuachia nyimbo nyingine
za 'Vululuvululu' na 'Changanyachanganya', amefariki Jumatatu ya Novemba
26 saa mbili usiku maeneo ya Maguzoni Muheza mkoani Tanga kwa ajali ya
gari akitokea Dar es Salaam.
LULU OSCAR
Pia ndani ya mwezi huohuo, aliyekuwa Mtangazaji wa Kipindi cha Pepeta Afrika kunako SibukaTV, Dar, Lulu Oscar alifariki ghafla akiwa nyumbani kwao Mbezi-Kwayusuf, Dar baada ya kuzidiwa kwa kubanwa na kifua.Lulu alikuwa mchangamfu na mcheshi mwenye kupenda sana utani, nilimfahamu awali akiwa mtangazaji katika radio moja kule Njombe, ambapo hatimae aliamua kuhamia Dar es Salaam kutafuta maisha na akapata kazi Sibuka TV.
Mungu Amlaze peponi pema Amen
AMINA SINGO

Mwezi Desemba, fani ya utangazaji nayo ilipata pigo baada ya kuondokewa na aliyekuwa Mtangazaji wa Kipindi cha Afro-Vibes cha Times FM, Dar, Amina Singo aliyekuwa akiugua kwa muda mrefu.
Uongozi wa bendi ya muziki wa dansi ya Extra Bongo ‘Next Level’
ulisema kifo cha aliyekuwa mtangazaji wa kituo cha Redio Times FM, Amina
Singo, ni pigo kubwa kwa tasnia ya muziki wa dansi na michezo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Bendi hiyo, Ally Choki, mtangazaji huyo alikuwa kiungo kikubwa kwa kupromoti muziki wa dansi ambao bado ulikuwa ukihitaji mchango wake.
Alisema wakiwa kama wadau wa muziki huo, wataendelea kumkumbuka marehemu kutokana na mchango wake alioutoa.
“Amina alikuwa ni mtu muhimu sana katika tasnia hii, sisi wanamuziki hatuna budi kuendelea kumkumbuka daima kutokana na vipindi vyake pia,” alisema Choki.
Alisema enzi za uhai wake, Singo alizipa nafasi kubwa bendi na wanamuziki wa dansi kujieleza kuhusu kazi zao, hali iliyofanya kazi zao za kimuziki kuendelea kusikika.
Mtangazaji huyo alifariki Jumapili na kuzikwa juzi maeneo ya nyumbani kwake Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
DAUDI MWANGOSI

IMEANDALIWA NA PAMOJA BLOG

Aliyekua mwandishi
wa habari wa Channel Ten mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa chama chama
cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Mpiganaji Marehemu Daud Mwangosi aliuwawa
katika vurugu za Polisi na wafuasi wa Chadema katika kijiji cha Nyololo
wilaya ya Mufindi mkoani Iringa leo.
Mwanahabari huyo Daud Mwangosi aliuwawa majira ya saa 10 jioni katika ofisi za Chadema Nyololo huku askari mmoja akiwa amejeruhiwa vibaya kwa risasi .
Kabla ya kuuwawa kwa mwanahabari huyo mabomu yalipigwa eneo hilo kuwatawanya wafuasi hao wa Chadema ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini na kudai kuwa hawapo tayari kuondoka katika ofisi yao.
Katika vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 kwa askari na wafuasi wa Chadema kurushiana mawe kwa mabomu magari kadhaa yaliharibiwa huku watu kadhaa walijeruhiwa, ikiwa ni pamoja na mwanahabari mmoja Godfrey Mushi wa NIPASHE.

No comments:
Post a Comment