Baadhi ya vijana wa eneo hilo wakijaribu kukwapua baadhi ya spea za gari hilo wakati likiungua.
GARI aina ya Toyota Starlet lenye namba za usajili T 382 BUN mali ya mwanamke mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake, limeteketea kwa moto muda huu nje kidogo ya ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam zilizopo Ilala – Boma. Kitendo cha ajabu ni kuona vijana waliokuwa eneo hilo baada ya kusaidia kuzima moto usiendelee kuliteketeza gari hilo, walionekana wakiwa ‘busy’ kung’oa baadhi ya spea za gari hilo.



No comments:
Post a Comment