Staa wa Vichekesho na Filamu Bongo, Said Mohamed Ngamba ‘Mzee Small’ akiwa amelazwa hospitali kutokana na maradhi yanayomsumbua.
KWENU mnaohusika na sanaa ya filamu Bongo. Mnajitambua sina haja ya kuwataja mmojammoja kwa majina, nitamaliza ukurasa bure.
Mimi
najua mpo poa, mnaendelea na majukumu yenu ya kila siku. Binafsi niko
poa, naendelea na majukumu yangu ya kila siku ikiwamo hili la
kuwaandikia barua.
Barua
yangu leo moja kwa moja nailekeza kwa nyinyi wote ambao watu sasa hivi
wanawatambua kwa jina la mastaa wa filamu katika soko la Bongo, Bongo
Movies.
Kikubwa
ni kwamba, natambua mchango mlionao katika kusogeza gurudumu la
maendeleo ya nchi. Natambua umuhimu wenu wa kuwatibu watu kisaikolojia
kupitia filamu zenu mnazozifanya.
Hongereni kwa hilo.Katika
taaluma yangu ya uandishi wa habari, mara kadhaa nimeshuhudia uwezo
wenu katika kufanikisha mambo yanayowahusu, iwe ni sherehe au misiba.
Eeeh,
kwenye sherehe basi mnalipuka na kushangweka kwelikweli. Kwenye misiba,
mnahakikisha mnamsindikiza mtu anayewahusu kwa hadhi anayostahili.
Hoja
hapa ni kwamba, hadhi ile ambayo mnajitutumua hadi kwenye misiba, kwa
nini tusioneshe kwa mkongwe wa sanaa nchini, Said Ngamba ‘Mzee Small’?
Tunashindwa nini? Mbona pesa zipo?
Kwa nini tusimsaidie mzee wetu ambaye tunaimani alikuwa chachu ya vijana wengi kuingia kwenye sanaa?
Mzee
wetu anasumbulia na ugonjwa wa kupararazi. Anashindwa kufanya shughuli
zake za sanaa ambazo ndiyo chanzo cha pato lake la kila siku.
Binafsi
nilisikitishwa na kupongeza kitendo cha Rais wa Shirikisho la Filamu
nchini TAFF, Saimon Mwakifwamba kuingilia kati na kuanza kutembeza
‘bakuli’ la michango kwa ajili ya kumsaidia mzee huyo.
Nilisikitika
kwani sikuona haja ya yeye kuingilia kati suala hilo ambalo naamini
lilikuwa chini ya uwezo wenu, mnaweza bwana! Kikubwa ni kipi haswa?
Mbona mna ‘mauwezo’, msinifanyie hivyo bwana.
Kwani
kuna tatizo gani tukiweka nukta katika starehe hata kwa siku moja,
tusipige kilevi siku hiyo halafu tujichangishe fedha za kumpa sapoti
mwenzetu kwenye kipindi hiki ambacho anaumwa?
Hakika hili ni dogo, tukiamua tunaweza tena haliwezi kuharibu bajeti zenu hata kidogo.
Ni yule yule,
Mkweli Daima.
Joseph Shaluwa
No comments:
Post a Comment