Amin Salmin
Adai si ndugu yao na hapaswi kutumia jina la Baba yake
MTOTO wa pili wa
Rais Mstaafu wa Serikali ya Zanzibar, Dk. Salmin Amour, Amin Salmin,
ameibuka na kukanusha vikali kuwa 'Ndugu Jambazi' Kassim Ramadhan Juma
(27) aliyeripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kukamatwa kwa ujambazi
kuwa si ndugu yao katika familia.
Akizungumza na Mtandao huu, Amin, alisema kuwa amesikitishwa sana
na kijana huyo aliyeripotiwa katika vyombo vya habari kwa tukio la
ujambazi kwa kutumia vibaya jina la Baba yake wakati si mtoto wa baba
yake na wala hakuzaliwa na Baba yake na pia na ndiyo maana anaita
Ramadhan Juma.
Aidha Amin alisema kuwa
wakati mama yake na mtoto huyo anayejulikana kwa jina la Salma Kasu,
alipokuwa akiolewa na Baba yake mwaka 1990, tayari mtoto huyo Kassim
Ramadhan Juma, alikuwepo na alikuwa ana umri wa miaka, 22 ambapo hadi
leo ana umri wa miaka 27.
''Wakati Baba yangu akimuoa
Mama yake na Ramadhan huyu kijana alikuwa na miaka 22, inamaana Baba
yangu alimkuta mama yake akiwa tayari na mtoto mkubwa tu, ambaye Mama
yake alizaa na mume mwingine kabla ya kuolewa na baba yangu,. sasa iweje
leo ajiite mtoto wa Salmin tena katika mambo yake mabaya yasiyofaa
katika Jamii, si kutaka kumchafua tu Mzee wa watu na kumpa mipresha ya
bure, baba yangu''?. alihoji Amin.
Kwa kubainisha usemi wake
Amin, aliongeza kuwa anawatambua vilivyo nduguze watatu, aliowataja kwa
majina, kuwa ni Abal, Hamoud na Salama, ambao wamezaliwa na mama wa
Kassim Ramadhan Juma, na Baba yake mzazi Dkt. Salmin Amour.
''Mimi nawatambua ndugu
zangu ambao Baba yangu amezaa na Mama wa Kassim Ramadhan Juma, Salma
Kasu, lakini huyu 'ndugu Jambazi' wala simtambui katika familia yetu, na
wala hajawahi kutokea kati yetu kutumia jina la baba kwa 'Ujina na
upuuzi' kama anavyofanya huyo ndugu Jambazi, Namuomba sana huyo Kassim
Ramadhan Juma, na wenzake wasiendelee kutumia jina la Baba yangu kwa
maovu yao kwani ni kutaka kumchafua tu baba yangu ambaye haitaji kuwa na
presha za namna hiyo kwa sasa''. alisema Amin
Chanzo: www.sufianimafoto.blogspot.com
No comments:
Post a Comment