Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Godbess Lema akipeana mkono na
aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama cha NCCR-Mageuzi (Bara) Lawrence
Surumbu Tara na Diwani wa kata ya Bashnet Wilayani Babati Mkoani
Manyara ambaye jana alitangaza kujivua udiwani na vyeo vyote
alivyokuwa navyo NCCR-Mageuzi na kujiunga na Chadema mjini Babati jana.
Picha na Joseph Lyimo
NI NAIBU KATIBU MKUU, LAWRENCE TARA, ATAJA SABABU LUKUKI, MBATIA AKUBALI YAISHE
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi,
Lawrence Tara, amejivua uanachama wa chama hicho na kuhamia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Tara ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Bashnet,
wilayani Babati, Mkoa wa Manyara tangu mwaka 2000, alitangaza uamuzi
huo mbele ya waandishi wa habari jana, baada ya kupokewa Chadema na
Mjumbe wa Kamati Kuu wa chama hicho, Godbless Lema.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na kiongozi mwingine wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini, Ally Bananga.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na kiongozi mwingine wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini, Ally Bananga.
Tara alitoa sababu mbili zilizomfanya aihame
NCCR-Mageuzi na kujiunga na Chadema; upendeleo na dhuluma kwa watumishi
wa chama hicho.
Alidai kwamba baadhi ya viongozi wa NCCR-Mageuzi wanaonyesha upendeleo wa wazi kwa kigezo cha urafiki kama kifanyavyo chama tawala, CCM.
Alidai kwamba baadhi ya viongozi wa NCCR-Mageuzi wanaonyesha upendeleo wa wazi kwa kigezo cha urafiki kama kifanyavyo chama tawala, CCM.
Alisema yeye ni mmoja wa waathirika wa mfumo huo
mbovu ndani ya NCCR- Mageuzi, baada ya chama hicho kumtelekeza katika
kudai haki yake ya ubunge aliyodai kwamba iliporwa na CCM.
“Tunahitaji chama cha siasa kilicho makini na
ambacho Watanzania tunapaswa kuunganisha nguvu zetu kwa pamoja bila
kutengana na kwa maoni yangu NCCR-Mageuzi siyo chama cha aina hiyo,”
alisema Tara.
Akifafanua madai ya kudhulumiwa na CCM, Tara alidai kwamba alishinda ubunge wa Jimbo la Babati Vijijini, lakini akadhulumiwa.
Alisema katika mazingira hayo amebakiwa na chaguo mojawapo kati ya kubaki ndani ya chama kisichokerwa na hali hiyo na ambacho baadhi ya viongozi wake wanaendeleza upendeleo wa urafiki na undugu.
Alisema katika mazingira hayo amebakiwa na chaguo mojawapo kati ya kubaki ndani ya chama kisichokerwa na hali hiyo na ambacho baadhi ya viongozi wake wanaendeleza upendeleo wa urafiki na undugu.
“Nikaona bora kujitenga na kuachana na chama
chenye viongozi wa aina hiyo na kutafuta chama imara ambacho hakina
simile na mambo kama hayo. Pia chenye kupigania haki, ukweli na ambacho
kimepania utawala bora na ustawi wa Watanzania,” alisema.
“Ninaamini Chadema ni chama makini kilichopania kutokomeza dhuluma, uovu na ufisadi wa kidola na kuleta ustawi wa Tanzania,” alisema na kuwaomba wakazi wa Bashnet, Manyara
“Ninaamini Chadema ni chama makini kilichopania kutokomeza dhuluma, uovu na ufisadi wa kidola na kuleta ustawi wa Tanzania,” alisema na kuwaomba wakazi wa Bashnet, Manyara
Watanzania kumuunga mkono.
Akizungumza katika mkutano huo, Lema alimpongeza Tara na kusema chama hicho sasa kimeongezewa nguvu.
“Huyu ni sawa na Leonel Messi (mchezaji soka
mahiri wa klabu ya Barcelona na Argentina). Sasa huwezi kumleta achezee
AFC ya Arusha na Babati Stars halafu mpate mafanikio kutokana na mfumo
uliopo, huyu anatakiwa awe Manchester United au timu nyingine kubwa,”
alisema Lema.
Alisema viongozi wa chama chake badala ya kumpa
ushirikiano ili aweze kushinda ubunge, Mwenyekiti wake alikubali kupewa
ubunge wa kuteuliwa na Rais na hivyo Tara kuachwa mwenyewe.
“Uso umeumbwa na haya kuna vitu ukishakula huwezi
kupinga. Hivyo jambo bora ni kuondoka huko na kwa hili nampongeza Tara
kwa kuacha vyeo vyote ikiwemo posho za vikao vya udiwani na posho ya
kila mwezi,” alisema Lema.
Alisema Tara anatarajiwa kupewa kadi ya chama
hicho na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe au Katibu Mkuu wake, Dk
Wilbroad Slaa kwa kuwa yeye hawezi kufanya hivyo kutokana na nafasi
kubwa aliyokuwa nayo mwanachama huyo mpya.
Mbatia amtakia heri, Ruhuza aduwaa
Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, James Mbatia alisema anamtakia kila la heri Tara, kwani Katiba ya nchi inamruhusu mtu yeyote kujiunga na chama anachokitaka.
“Unajua kila neno linazaa neno. Hilo la kusema hatukumpa ushirikiano wakati wa kesi yake ni wazo lake. Namtakia kila la heri huko alipokwenda kwani yeye ana uhuru wa kujiunga na chama chochote. Kama anaona kile anachotaka anaweza kupata sehemu nyingine, aende hakuna tatizo,” alisema Mbatia.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Samweli
Ruhuza alionyesha kushangazwa na hatua hiyo ya Tara alisema kuwa,
alikuwa katika nafasi nzuri ya kushinda ubunge wa Babati Vijijini kwa
njia ya Mahakama kupitia chama hicho.
“Sijawasiliana naye. Nimeona tu kwenye mtandao
kwamba amehamia Chadema, lakini ni haki yake kwa vile ana haki ya
kuhamia chama chochote,” alisema Ruhuza.
Alisema kitendo cha kada huyo kusema amehama kwa kuwa chama kilimtelekeza, ni uongo kwa kuwa NCCR kilimlipia kila kitu katika kesi yake ya kuwania ubunge wa Babati Vijijini na hata kumpa gari ambalo analitumia hivi sasa.

“Aligombea ubunge na udiwani pale Babati Vijijini,
lakini alishinda udiwani na kushindwa ubunge, kwa kuwa tafiti zetu
tulizofanya alishinda, tulimlipia wakili asimamie kesi ya kupinga
matokeo ambayo inaonyesha angeshinda,” alisema Ruhuza.
Alisema ameshangazwa zaidi na kauli yake ya
kutelekezwa na chama wakati akiwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa,
pia ni Naibu Katibu Mkuu wa chama.
“Huyo amekosa kila kitu, ubunge ambao angeweza
kuupata kwa njia ya Mahakama, Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu na nyinginezo.
Ingekuwa ninaamini mambo ya uchawi ningesema labda huyo jamaa
amerogwa,” alisema Ruhuza na kuongeza:
“Hata gari la chama aina ya Double Cabin analotumia itabidi alirudishe baada ya kujiondoa kwenye chama.”
CHANZO: MWANANCHI
“Hata gari la chama aina ya Double Cabin analotumia itabidi alirudishe baada ya kujiondoa kwenye chama.”
No comments:
Post a Comment