Kocha wa ngumi Pascal Mhagama (kushoto) akimfua bondia Mbwana Matumla kwa ajili ya mpambano wake na David Chalanga wa Kenya mpambano utakaochezwa Desemba 25 katika ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem.
Kocha wa Mchezo wa Masumbwi Said Chaku (kushoto) akimwelekeza bondia Mada Maugo jinsi ya kutupa masumbwi wakati wa mazoezi yake ya mwisho kwa ajili ya kumkabili bondia Yiga Juma wa Uganda mpambano utakaofanyika Desemba 25 katika ukumbi wa Dar Live jijini Dar es Salaam.
Bondia Mbwana Matumla (kushoto) akionesha ufundi wa kutupa masumbwi mbele ya kocha wake Pascal Mhagama kwa ajili ya mpambano wake na David Chalanga wa Kenya kwenye mpambano utakaochezwa Desemba 25 katika ukumbi wa Dar Live.
Bondia Mada Maugo (kushoto) akionesha umahiri wa kutupa makonde na kocha wake Said Chaku wakati wa mazoezi yake ya mwisho kabla ya kupambana na bondia Yiga Juma wa Uganda Desemba 25 katika ukumbi wa Dar Live jijini Dar es
Salaam.
Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
No comments:
Post a Comment