Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa Injinia Stella Manyanya akikabidhi zawadi za skukuu ya krismas na
mwaka mpya 2013 kwa watoto yatima wa kituo cha Bethania mjini
Sumbawanga. Katika msimu huu wa Skukuu Mkuu huyo wa Mkoa ameamua
kusherehekea kwa kuwatembelea watoto yatima na wafungwa wa gereza
mahabusu Sumbawanga na gereza la Mollo kwa kuwapa chakula cha skukuu
pamoja na kuskiliza kero zao mbalimbali. Zawadi
alizotoa ni Mbuzi, Mchele pamoja na sabuni za kufulia kwa watoto yatima
wa kituo cha Bethania vikiwa na thamani ya Tsh. 380,000/=
Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa Injinia Stella Manyanya akiwa kwenye picha ya pamoja na watoto
yatima wa kituo cha Bethania Mjini Sumbawanga waliofaulu na kuchaguliwa
kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2013 katika shule mbalimbali Mkoani
Rukwa. Mkuu huyo wa Mkoa ameahidi kugharamia masomo yao kwa kidato cha
kwanza na sare za shule pamoja na vitendea kazi vingine. Kulia ni Kaimu
Katibu Tawala wa Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Festo Chonya akimuwakilishha
Mkuu wa Wilaya hiyo Ndugu Methew Sedoyyeka.
Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa Injinia Stella Manyanya akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya
watoto yatima wa kituo cha Bethania Mjini Sumbawanga alipowatembelea
kuwafariji kwa chakula katika msimu huu wa sikukuu.
Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa akizungumza na watoto yatima wa kituo cha Bethania, kulia ni Mkuu
wa kituo hicho Ndugu Emmanuel Mwampimbwe. Mkuu huyo wa Mkoa aliagiza
watoto yatima katika kituo hicho pamoja na vituo vingine watambuliwe na
watengenezewe vitambulisho vitakavyowawezesha kupatiwa huduma bure
katika hospitali za Serikali Mkoani Rukwa.
Ndugu ASP. A. Kimati
akisoma taarifa ya gereza la Mollo kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia
Stella Manyanya alipotembelea gereza hilo jana kutoa salamu na chakula
cha sikukuu kwa wafugwa wa gereza hilo na kuskiliza kero zao mbalimbali.
Mkuu huyo wa Mkoa alipokea kero mbalimbali kutoka kwa wafugwa 195 wa
gereza hilo ikiwemo uhaba wa sare za wafungwa, wafugwa kutopewa nakala
za hukumu zao, kesi zao kusikilizwa kwa kiswahili lakini hukumu
kuandikwa kiingereza, kutokukubalika kwa dhamana zao, kutokuwepo kwa
hakimu katika Wilaya ya Nkasi, na baadhi ya kesi kuchelewa kuskilizwa.
Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa Injinia Stella Manyanya akijumuisha ziara yake gerezani Mollo kwa
kuzungumza na viongozi wa Jeshi la Polisi na Jeshi la magereza Mkoani
humo ambapo aliahidi kufuatilia kero zote zilizowasilishwa kwa
kushirikiana na pande zinazohusika kuhakikisha zinapatiwa ufumbuzi.
Alisema kuwa ataendelea kuweka msukumo wa ujenzi wa mahakama za Nkasi na
Wilaya mpya ya Kalambo. Aidha aliutaka uongozi wa gereza hilo kufyatua
matofali kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wafungwa katika gereza hilo
ambapo yeye atasaidia upatikanaji wa mabati na vifaa vingine vya
madukani, kwa sasa mabweni yanayotumika katika gereza hilo ni ya mabati
magumu ambayo kutokana na hali ya hewa ya maeneo hayo kunakuwa na baridi
kali kwenye msimu wa baridi.
PICHA NA OFISI YA MKUU WA MKOA RUKWA
No comments:
Post a Comment