Kuta za jengo hili zimepabwa na kila aina ya lugha za kejeli na matusi kwa walimu.
NI takriban Kilometa 60 kutoka Ikwiriri hadi
kufika iliko Shule ya Sekondari Ruaruke iliyopo Kata ya Ruaruke Wilaya
ya Rufiji, mkoani Pwani.
Usafiri wa kuaminika kuelekea huko ni pikipiki ambazo pamoja na kuwa nauli yake ni ghali, ndio unaoweza kukufikisha huko.
Ili ufike Ruaruke utalazimika kupita katika vijiji
vya Mchukwi A, Mchukwi B na Nyamatanga. Shule hiyo ipo kati ya vijiji
vya Ruaruke A na Ruaruke B.
Safari yangu ya kuelekea katika shule ya sekondari
ni taarifa zilizochapishwa na gazeti hili hivi karibuni, kuhusu hali
ya kusikitisha inayowakabili walimu wa shule hiyo iliyojengwa kwa nguvu
za wananchi kuanzia mwaka 2001 na kukamilika 2004.
Shule ya Sekondari Ruaruke imekuwa ikipokea wanafunzi wa vijiji mbalimbali vya Kata ya Ruaruke na kata nyingine za jirani.
Wakazi wengi wa Kata ya Ruaruke ni wakulima na
wafanyabiashara ndogondogo. Kilimo kikuu eneo hilo ni pamoja na muhogo,
mpunga, mahindi na mazao jamii ya kunde.
Hata hivyo, wakazi wengi wanaisha maisha duni, kiasi kwamba ni familia chache zinazomudu kula milo mitatu kwa siku.
Hata hivyo, wakazi wengi wanaisha maisha duni, kiasi kwamba ni familia chache zinazomudu kula milo mitatu kwa siku.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Ruaruke A, Suleiman
Mfaume anasema kwa sababu wanafunzi wengi wanaishi mitaani
wakijitegemea, ni vigumu kubaini na hata kudhibiti mienendo yao
isiyofaa.
“Uvutaji bangi na ngono ni jambo lisiloepukika kwa baadhi ya vijana, kwani hakuna wa kuwalinda kutokana na wao kuishi wakiwa huru bila ulinzi wa wazazi wao, “anaeleza.
“Uvutaji bangi na ngono ni jambo lisiloepukika kwa baadhi ya vijana, kwani hakuna wa kuwalinda kutokana na wao kuishi wakiwa huru bila ulinzi wa wazazi wao, “anaeleza.
Unapofika shuleni hapo na kutupa jicho katika baadhi ya kuta za majengo, ukionacho kinatosha kukupa picha halisi ya aina ya wanafunzi wanaosoma hapo.
Kwa mfano, baadhi ya kuta sasa zimepambwa na kila
aina ya michoro ya kudhalilisha, lugha za kejeli, maudhi na hata matusi
kwa walimu hasa Mkuu wa Shule ambaye katika maandishi mengi ukutani
amekuwa akitajwa kwa jina la Ngozi.
Baadhi ya matusi hayaandikiki gazetini, lakini kwa
kuta za Shule ya Sekondari Ruaruke, hilo limewezekana. Walioandika bila
shaka walifanya hivyo kuonyesha hisia zao kwa mtu wanayemtaja kuwa
ndiyo adui yao.
Miongoni mwa maandishi hayo, kulikuwa na haya yaliyosema: ‘baada ya mwalimu mkuu bado mwalimu Moyanga’
Kwa kuwa ziara yangu niliifanya siku chache baada
ya vurugu kutokea shuleni hapo, macho yangu hayakusita kuona mabaki ya
viti vilivyoharibiwa madarasani, nyumba ya mwalimu mkuu iliyovunjwa na
majengo yaliyochomwa moto.
Walimu waikimbia shule
Taarifa za awali zilizoandikwa na gazeti hili zinasema walimu waliamua kuikimbia shule hiyo baada ya kukithiri kwa vitenda vya unyanyasaji kimapenzi kwa walimu wa kike na vitisho.
MWANANCHI
Kwa hakika shule ilikuwa imetelekezwa, mazingira yake hayavutii
kuyatazama. Kukosekana kwa watu wanaoishi hapo, kumetoa mwanya kwa
majani kuota kwa kasi katika eneo la shule kiasi cha kusababisha pori la
aina yake.
Kitaaluma hali si nzuri katika shule hiyo. Kwa
mfano, katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2011 wahitimu
74 kati ya 91 walipata daraja sifuri, 14 walipata daraja la nne.
Taarifa za awali zilizoandikwa na gazeti hili zinasema walimu waliamua kuikimbia shule hiyo baada ya kukithiri kwa vitenda vya unyanyasaji kimapenzi kwa walimu wa kike na vitisho.
Aidha, taarifa zilieleza kwamba walimu hao
walilazimika kuikimbia shule hiyo baada ya baadhi ya walimu wa kike
kutongozwa na wanafunzi,kubakwa, kupigwa mabusu kwa nguvu hadharani,
kutishiwa kuchomwa visu na kuchorwa vikatuni vya kudhalilisha.
Baadhi ya walimu, watendaji wa kata, Mkuu wa
Wilaya ya Rufiji na Mbunge wa Kibiti walithibitisha ukweli wa suala
hilo walilosema wanalifahamu na kwamba wapo kwenye mchakato wa
kulipatia ufumbuzi.
Wanafunzi wazungumza
Mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo anayesoma kidato cha tatu, (jina tunalihifadhi) anasema kwanza ieleweke kuwa vurugu hazikusababishwa na wanafunzi wachache wanaotuhumiwa.
Mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo anayesoma kidato cha tatu, (jina tunalihifadhi) anasema kwanza ieleweke kuwa vurugu hazikusababishwa na wanafunzi wachache wanaotuhumiwa.
Hatua ya kufanya fujo anasema ilitokana na uamuzi
wa wanafunzi wote baada ya kuchoshwa na vitendo vya unyanyasaji
walivyokuwa wakifanyiwa na walimu. Anasema hata pale baadhi yao
walipowashtaki walimu hao katika bodi ya shule, hakuna hatua
zilizochukuliwa. “… shule nzima hivyo ni vyema shule nzima ikashitakiwa
kwa kuwa wanafunzi waliamua wote kufanya vurugu. Kushitakiwa watu
wachache ni kuwaonea,’’anasema na kuongeza:
“Sababu kubwa ya kufanya vurugu ni tabia ya walimu
kutupiga kwa kutumia ngumi, mateke na kutoingia madarasani na walimu
kutoa adhabu kali wakati madarasani hawaingii, bali wanatoa notisi tu,
Walimu wamekuwa wakali sana na wamekuwa wakitoa adhabu kali wakati
madarasani hawaingii, hivyo sisi tukaona njia mwafaka ni kufanya vurugu
ili kukomesha unyanyasaji huo.’’
Dai lao lingine wanafunzi hao wanasema ni shule kukosa walimu wa sayansi kwa muda mrefu.
Hata hivyo, uchunguzi wa Mwananchi umebaini tabia mbaya za baadhi ya wanafunzi, zina baraka za wazazi wao wanaoshindwa kuwakemea.
Hata hivyo, uchunguzi wa Mwananchi umebaini tabia mbaya za baadhi ya wanafunzi, zina baraka za wazazi wao wanaoshindwa kuwakemea.
Kibaya zaidi wazazi hao huja juu pale watoto wao wanapoadhibiwa na walimu.
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment