Mkurugenzi wa Kampuni ya Meli ya MV. SAMAR Salum
Ally akizungumza na vyombo vya habari. ABIRIA na wananchi wanaotumia kivuko cha MV. SAMAR wamepinga vikali agizo la Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt. Charles Tizebar la kuamuru kusitishwa kwa huduma ya usafiri wa kivuko hicho kinachotoa huduma kati ya Mwanza mjini na Kamanga Wilayani Sengerema hali iliyopelekea wananchi kupinga vikali hatua hiyo ya Naibu Waziri na Serikali.
Wananchi
na abiria hao wamesema kwamba kauli hiyo ya Naibu Waziri Dkt.Tizebar
aliyoitoa hivi karibuni wakati wa kuipokea treni ya abiria ya kutoka
Jijini Dar es salaam hadi Jijini Mwanza kuwasili kwa mara ya kwanza
tangu kuanza kazi Desemba 9 mwaka huu baada ya kusitisha safari zake kwa
miaka mitatu kwa madai kuwa wamezuia njia ya reli iendayo bandarini
huku madai hayo yakionekana kupingana na Mamlaka ya Bandari ya Mwanza
Kaskazini waliodai kuwa kwa sasa hawahitaji huduma ya Treni kufika
Bandari hiyo na ni miaka zaidi ya kumi Treni kupita na kufika Bandari
hiyo ya Mwanza Kaskazini.
Akizungumza
na vyombo vya Habari Mkurugenzi wa Kampuni ya Meli ya MV. SAMAR Salum
Ally alisema kwamba agizo la kusimamisha huduma na kuhamia eneo la
maegesho ya Meli za Marine Service huku kukiwa hakuna matayarisho ya
barabara ya magari kuingia na kutokea,abiria na daraja la meli hiyo
kuweka nanga ili kuruhusu abiria na magari kupita kirahisi kama ilivyo
kwenye eneo kilipokuwa kikitolea huduma awali.
Salum
amesema kwamba alipokea barua ya kwanza ya Mamlaka ya Bandari ya
Kaskazini (PTA) Desemba 11 mwaka 2012 yenye kumb.MN/2/3/04 iliyosainiwa
na Mkuu wa Bandari hiyo Mhandisi Josephat Mutalemwa huu ikisomeka
kwamba ‘AGIZO LA NAIBU WAZIRI LA KUHAMISHA HUDUMA YA KIVUKO KUTOKA HAPO
ULIPO NA KUELEKEA NDANI ZAIDI YA BANDARI YA KASKAZINI’ ikiwa ndani ya
wiki tatu za kutekelezwa kwa agizo hilo.
Barua ya kwanza.
Ameongeza
kuwa wakati akitafakali juu ya uamuzi huo wa barua hiyo na Agizo la
Naibu Waziri Dkt.Tizebar,Kabla ya wiki moja kumalizika ghafla akapokea
barua nyingine tena ya pili ambayo pia ikitolewa na PTA Desemba 19 mwaka
huu na ikisainiwa na Kaimu Mkuu wa Bandari T.S.Akile iliyosemeka
'KUSITISHA HUDUMA YA KIVUKO KUTOKA HAPO ULIPO NA KUELEKEA ZAIDI NDANI YA
BANDARI YA KASKAZINI' Mamlaka ya usimamizi wa Bandari (PTA) inakutaka
kusitisha mara moja shughuli za kupakia na kushusha abiria na mizingo
kuanzia sasa hivi (Leo Desemba 19 mwaka huu).
Kufatia
hatua hiyo hali ilikuwa tofauti kwa wananchi na abiria na kuanza
kurusha mameno na kauli kali za kupinga hatua ya PTA,Serikali na Agizo
la Naibu Waziri Dkt. Huku Mkurugenzi wa SAMAR alidai kuwa ameheshimu
kauli ya Waziri na agizo la barua za PTA, akidai kuwa amekuwa akiilipa
PTA kiasi cha shilingi milioni 2 kwa mwezi ikiwa ni makubaliano baada ya
kuomba kutumia eneo hilo na kupitia Meli zake amekuwa pia akiliingizia
shirika hilo kiasi cha zaidi milioni 70 kwa mwezi kwa huduma ya Bandari
ya Mwanza Kaskazini na Kusini.
Mbali na kuiingizia PTA mapato hayo, kampuni hiyo imekuwa akisaidia wanawake wajane zaidi 60 kiasi cha shilingi 600,000 kwa mwezi waliopo eneo la Kamanga huku serikali ya Kijiji hicho cha Kamanga kikiingiza kila siku kiasi cha elfu 40,000/= ikiwa ni huduma za wananchi wanaotumia vyoo katika eneo la kugota Meli ya MV. SAMAR huku wanafunzi wote wakipita bure katika kivuko hicho wakiwemo wazee wa zaidi ya miaka 70 na mama wajawazito na watoto walio chini ya miaka 8 kila siku ya huduma wa Meli hiyo.
Mbali na kuiingizia PTA mapato hayo, kampuni hiyo imekuwa akisaidia wanawake wajane zaidi 60 kiasi cha shilingi 600,000 kwa mwezi waliopo eneo la Kamanga huku serikali ya Kijiji hicho cha Kamanga kikiingiza kila siku kiasi cha elfu 40,000/= ikiwa ni huduma za wananchi wanaotumia vyoo katika eneo la kugota Meli ya MV. SAMAR huku wanafunzi wote wakipita bure katika kivuko hicho wakiwemo wazee wa zaidi ya miaka 70 na mama wajawazito na watoto walio chini ya miaka 8 kila siku ya huduma wa Meli hiyo.
Kivuko
hicho cha MV.SAMAR kinacho beba abiria wapatao 390 kwa wakati
mmoja,mizigo tani 320 kwa kila safari moja ifanyayo ambapo kwa kutwa
nzima ni zaidi ya abiria zaidi ya 3,500 kwa siku nzima ya safari 12 za
abiria na mizigo kutoka Jijini Mwanza hadi Kamanga Wilayani Sengerema
tangu kukubaliwa na Uongozi wa Mamlaka ya Bandari ya Mwanza Kaskazini
Septemba 17 mwaka huu hadi Septemba 17 mwaka 2013 ikiwa ni mkataba wa
majaribio wa mwaka mmoja kabla ya kusainiwa mkataba mwingine.
Njia
ya reli ndani ya eneo ambayo kimsingi kwa upande wa wamiliki wa eneo la
kivuko cha MV. SAMAR ambao wao wameacha nafasi ya kutosha kwa reli hiyo
kupitika zaidi ya kutumia eneo la reli kama sehemu ya barabara
ikatishayo kwa ajili ya magari.
![]() |
Baadhi ya abiria walikuwa wakitakiwa kupanda kivuko husika wakirejea kwenye siti zao kufanya mgomo wa kulazimisha safari ziendelee. |
Ghati
ya eneo ambalo huduma inapaswa kuhama kufuatia agizo la kusimamisha
huduma na kuhamia eneo la maegesho ya Meli za Marine Service
Mishemishe za biashara eneo la Kamanga ferry.
PICHA NA KAJUNASON BLOG
No comments:
Post a Comment