Wasanii wakisalimiana na Rais walipoingia ikulu
wasanii wakizungumza na Rais ikulu leo
Jopo la wasanii mahiri leo limefika Ikulu kumshukuru Rais kwa mambo mengi ambayo amewafanyia wasanii katika mwaka huu unaoisha. Katika msafara huo, wanamuziki walitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais kwa kuwapa tuzo za heshima wasanii wakati wa sherehe za miaka 51 ya Uhuru. Wasanii pia walichukua nafasi hiyo kumshukuru Rais kwa kuwajali wakati wa shida kama kuhudhuria misiba, kusaidia wagonjwa na kadhalika.
Wasanii waliokuweko katika msafara huo ni;
Waziri Ally,Abdul Salvador, Cosmas Chidumule, Hamis Mwinjuma (Mwana FA),Hamza Kalala, King Kiki, Ado Mwasongwe, Shakila Said, Simon Mwakifwamba, Carola Kinasha, Ruge Mtahaba, Chiki Mchoma.
No comments:
Post a Comment