Bodaboda wapambana na polisi Mwanza

Vurugu kubwa zilitokea mwanza  kati ya polisi na wenye boda boda, milio ya mabomu na risasi zilipigwa na kusikika  eneo la makongoro mission jijini mwanza..  Huduma za usafiri zilisimama barabara ya kuelekea Airport jijini Mwanza baada ya Polisi kutumia risasi za moto na za machozi kuwakabili waendesha pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda kwa kukiuka sheria. Hivyo kutokana na mvutano  huo  jeshi la  polisi  limelazimika  kutumia risasi  za moto  kuwafukuza  waendesha boda  boda  hao na kuna taarifa   kuwa baadhi yao  wamejeruhiwa vibaya katika  vurugu  hizo .

 
 Maasikari wakiwa kazin ili kurudisha hali ya amani
 
 Maasikari wakiingiza pikipiki kwenye gari wakati wa vurugu iliyotokea Mwanza hapo jana
 Askari wajeshi la polisi katika harakati ya kutawanya waandamanaji kwa njia ya mabomuya machozi eneo la Mission Makongoro Kirumba jijini Mwanza.

POLISI mkoani Mwanza wamelazimika kutumia risasi za moto na mabomu ya machozi kuwatawanya waendesha bodaboda waliokuwa wakiwalazimisha askari wawaachie wenzao waliowakamata kwa makosa mbalimbali.
Wakati hayo yakitokea Mwanza, huko Arusha, madereva teksi walipandwa na jazba baada ya kuzuka kwa mzozo kati yao na uongozi wa Hoteli ya Palace kutokana na kile walichoeleza kuwa ni kuondolewa kinyemela katika eneo lao.
Huko Mwanza, ghasia hizo ziliibuka wakati polisi wa usalama barabarani na kikosi maalumu cha ukaguzi wa magari walipofanya doria kukagua leseni na uhalali wa madereva hao wanaofanya shughuli za kusafirisha abiria.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, vurugu hizo zilianza saa 2:46 asubuhi baada ya polisi kuwakamata waendesha bodaboda wapatao 26, ambao walitozwa faini za papo kwa papo kulingana na makosa yao, huku wengine wakiendelea kushikiliwa.
Hatua hiyo iliwafanya waanze kujikusanya kutoka sehemu mbalimbali na kuandamana hadi eneo kulikokuwa limetengwa kwa ukaguzi huo katika Mtaa wa Mission.

Baada ya kufika eneo hilo, walianza kuwarushia mawe askari hao, huku baadhi yao wakiendesha pikipiki kuzunguka eneo hilo na kuzuia magari kupita hali iliyozua tafrani. Baada ya kutokea hivyo, askari hao walilazimika kuwaita askari wengine ili kuwakabili vijana hao.

Vurugu hizo zilizodumu kwa saa tatu, zilisababisha kufungwa kwa barabara iendayo Uwanja wa Ndege na katika eneo la Pasiansi, huku baadhi ya abiria wakilazimika kuteremka katika daladala na kukimbia ovyo na wengine kulala katika mifereji ya maji machafu baada ya milio ya risasi na mabomu ya machozi kuanza kurindima.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ernest Mangu alisema jana kwamba polisi hao walikuwa katika ukaguzi wa leseni na vifaa vingine vya usalama kama kofia ngumu ndipo baadhi ya madereva hao wa bodaboda wakaanza kupinga kukamatwa kwa wenzao na kutozwa faini kutokana na makosa waliyokuwa nayo.

No comments

Powered by Blogger.