.
Staa wa muziki Africa ambae
siku kadhaa zilizopita aliwahudumia mashabiki wake kwa kuwapa muziki juu
ya stage tatu tofauti Tanzania Koffi Olomide anatafutwa na polisi wa
Zambia.
Polisi Zambia wametangaza
kumsaka Koffi Olomide popote alipo nchini humo baada ya kuwatukana
walipojaribu kuingilia ugomvi wake na mmoja wa waandishi wa habari.
Inadaiwa Koffi alizinguana na
mwandishi huyo wa habari wakati akifanya moja kati ya showz alizopangiwa
nchini Zambia, hii sio mara ya kwanza kuingia kwenye matatizo na polisi
Zambia, miaka miwili iliyopita aliwaponyoka polisi kwa kutumia
pikipiki baada ya mzozo na promota wa show yake, kwa sasa polisi
wanasema kuna ushahidi wa kutosha kabisa wa kumkamata Koffi ambapo mkuu
wa Polisi kwenye mji wa Lusaka wamesema watafanya kila kinachowezekana
kumkamata Koffi ili akajibu hayo mashtaka.
Msemaji wa polisi Zambia Ndandula Siamana.
Promoters wake nchini Zambia
wanasema Koffi ameshaondoka Zambia tayari lakini polisi wanasema hawana
uhakika kama kweli kaondoka.
Kwenye line nyingine baadhi ya
vyombo vya habari nchini Zambia vilitangaza taarifa za Koffi kuonekana
kumpiga vibao mmoja wa wacheza show wake wa kike wakiwa backstage.
Nyumbani kwao Congo Koffi
Olomide mwenye umri wa miaka 58 alipelekwa mahakamani mwaka jana kwa
kosa la kumpiga na kumuumiza producer wake Diego Music Lubaki na
kuharibu vitu mbalimbali kwenye hoteli ugomvi ulipotokea mwezi August
mwaka jana.



No comments:
Post a Comment