WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda
AAHIDI NEEMA YA VIWANDA,WENYEJI WAMSHANGILIA,RC AOMBA RADHI
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amefanikiwa kutuliza
jazba za wakazi wa Mkoa wa Mtwara baada ya kueleza jinsi
watakavyonufaika na gesi itakayozalishwa mkoani humo kabla ya
kusafirishwa kwa bomba hadi Dar es Salaam.
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Joseph Simbakalia
amewaomba radhi wananchi wa mkoa huo kutokana na kauli Desemba 21, mwaka
jana akiwakebehi baada ya kumwomba apokee maandamano yao ya kupinga
mpango wa kusafirisha gesi hiyo.
Akizungumza katika mkutano wa majumuisho
uliofanyika jana baada ya kusikiliza madai ya wananchi hao kwa siku
mbili mfululizo, Pinda alisema hakuna tone la gesi ghafi
itakayosafirisha kwa njia ya bomba na kusema kiwanda cha kusindika gesi
ghafi kitajengwa katika Kijiji cha Madimba, mkoani humo ili mabaki
yatokanayo na gesi hiyo yatumike kuvutia uwekezaji wa viwanda.
“Wataalamu wanasema gesi haiwezi kwa namna yoyote
ile kusafirishwa kama ilivyo, lazima ibadilishwe kuwa hewa au barafu…
kiwanda cha kusafisha gesi kitajengwa Madimba. Gesi yote itakayotoka
Mnazi Bay itasafishwa hapo na masalia yote yatabaki huku ili kuvutia
viwanda vya mbolea na vingine vinavyotumia malighafi hizo,” alisema
Pinda na kuongeza:
“Kama tungekuwa tunasafirisha gesi ghafi basi hata
kiwanda cha Dangote kisingejengwa hapa… gesi itakayopelekwa Dar es
Salaam ni ile iliyosafishwa kwa ajili ya matumizi ya kuzalisha umeme…
tusaidieni wenzetu kuliokoa Taifa na tatizo la umeme.”
“Gesi lazima isindikwe Mtwara, haitoki hadi
viwanda vije… nadhani hili ni jambo jema lazima tuliwekee utaratibu.
Nikawauliza wataalamu wangu kwani kiwanda cha kusafisha gesi kinajengwa
wapi, wakanijibu Madimba… nikasema kumbe tatizo kubwa ni kutowaeleza vya
kutosha wananchi suala la gesi.” alisema Waziri Mkuu huku akipigiwa
makofi... “Nafikiri tatizo ni sisi Serikali hatukuwa na mpango mzuri wa
kuwaelimisha wananchi.”
Awali, madai ya wakazi wa Mkoa wa Mtwara yalikuwa
ku pinga usafirishaji wa gesi ghafi kwenda Dar es Salaam wakieleza kuwa
mpango huo utafukuza uwekezaji wa viwanda mkoani humo ambao ungechochewa
na upatikanaji wa malighafi baada ya kusafishwa kwa gesi.
Pia wananchi walipinga uje nzi wa mitambo ya
kuzalisha umeme Kinyerezi, Dar es Salaam wakiitaka Serikali kujenga
mitambo hiyo mkoani Mtwara.
Alitoa wito kwa wabunge wa Mkoa wa Mtwara kufuta
tofauti zao za kisiasa ili waweze kuharakisha maendeleo ya mkoa huo...
“Purukushani hizi ndani ya chama hazina tija, tuseme basi… wabunge
hawaelewani, sasa bungeni wanakwendaje... kila mtu na lake … hebu tuseme
watu kwanza mimi badaaye,” alisema Pinda huku akishangiliwa.
Katika siku hizo mbili mkoani Mtwara, Waziri Mkuu
alikutana na viongozi wa vyama vya siasa, dini, wafanyabiashara,
madiwani na wenyeviti wa mitaa na wanaharakati mbalimbali.
RC aomba radhi
Katika hatua nyingine, Mkuu wa Mkoa, Simbakalia aliwaomba radhi wakazi wa Mkoa wa Mtwara akisema alipotoka kuwaita wananchi hao wapuuzi na baadaye wahaini kauli ambazo ziliwaudhi wengi
RC aomba radhi
Katika hatua nyingine, Mkuu wa Mkoa, Simbakalia aliwaomba radhi wakazi wa Mkoa wa Mtwara akisema alipotoka kuwaita wananchi hao wapuuzi na baadaye wahaini kauli ambazo ziliwaudhi wengi
“Kupitia hadhara hii nawaomba radhi kwa kuwakwaza,
nimesikitishwa kwa kauli yangu ambayo imepokewa kwa hisia kwamba
niliwadharau,” alisema Simbakalia.
Baadaye Waziri Mkuu aliwasihi wananchi wa Mtwara
kumsamehe Mkuu wao wa Mkoa wa Mtwara kwa kauli hiyo aliyoitoa 21
Desemba, mwaka jana katika kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa, (RCC), pale
alipoombwa kuyapokea maandamano ya wakazi wa mkoa huo Desemba, 27,
mwaka jana.
Wenyeji waridhika
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa vyama tisa vya siasa mkoani Mtwara, Uledi Abdallah alisema madai ya wananchi yalikuwa mitambo ya kusafisha gesi ghafi ijengwe Mtwara na kwamba iwapo Serikali imeamua kufanya hivyo madai yao yatakuwa yamekwisha.
“Kama gesi itakayosafirishwa kwenda Dar es Salaam ni ile iliyosafishwa, sisi hatuna tatizo,” alisema Abdallah
Mbunge wa Mtwara Mjini (CCM), Hasnain Murji alimpongeza Waziri Mkuu kwa hatua yake ya kuwasikiliza wananchi na kwamba mzozo huo uliodumu kwa takriban mwezi mmoja sasa umefikia tamati.
Katibu wa Chama cha Wananchi (CUF), Mtwara Mjini, Saidi Kulaga alimpongeza Waziri Mkuu kwa hatua aliyoichukua na kumwomba awaachie huru wale waliokamatwa kutokana na vurugu zilizotokea Mtwara na Masasi ili kujenga mwanzo mpya wa uhusiano baina ya Serikali na wananchi, ombi ambalo Pinda alilipokea na kuahidi kulifanyia kazi ndani ya wiki mbili.
Wataalamu wa gesi
Awali, kutokana na vurugu hizo, zaidi ya wataalamu 50 waliokuwa mkoani Mtwara kwa ajili ya kusimamia mradi wa ujenzi wa bomba la gesi waliondolewa mkoani humo, Mwananchi limebaini.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili jana zilieleza kuwa watalaamu hao wapo Dar es Salaam tangu Jumamosi iliyopita na wamefikia katika Hoteli ya JB Belmont kupisha vurugu za wananchi waliokuwa wakipinga ujenzi wa bomba hilo kutoka mkoani humo kwenda Dar es Salaam.
Mmoja wa viongozi wa hoteli hiyo, ambaye alikataa kutaja jina lake kwa maelezo kuwa si msemaji alikiri kuwapo kwa watalaamu hao katika hoteli hiyo… “Wapo ila walisema kuwa hawa taki kuzungumza na vyombo vya habari.”
Bunge laingilia kati
Spika wa Bunge, Anna Makinda ameunda kamati itakayokwenda Mtwara kuzungumza na kada mbalimbali kuhusu vurugu na mustakabali mzima wa gesi.
Makinda alisema hayo jana muda mfupi kabla ya kuahirisha kikao cha kwanza katika Mkutano wa 10 wa Bunge… “Bunge ni chombo cha amani, tutawatuma wabunge kwenda kuzungumza nao…suala hili linahitaji busara sana.”
Habari hii imeandikwa na Abdallah Bakari (Mtwara), Fidelis Butahe (Dar), Ibrahim Bakari na Habel Chidawali (Dodoma)
MWANANCHI
“Binadamu kukosea lazima, lakini kubwa zaidi ni kuomba msamaha…
amefanya hivyo, sasa tusahau yaliyopita tugange yajayo,” alisema Pinda.
Mawaziri wazungumza
Akizungumzia hali ya usalama mkoani huo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi alisema wizara yake imejipanga vyema kukabiliana na vurugu zozote zitakazojitokeza kuanza sasa.. “Hali ni shwari, tumejipanga vya kutosha kwa watu na vifaa.”

Kwa upande wake, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi Dk Shukuru Kawambwa alisema wizara yake imeamua kuifanya Veta
Mtwara kuwa kituo cha umahiri ili wahitimu wake waweze kuajiriwa katika
sekta ya gesi huku Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Profesa Anna Tibaijuka akisema wizara yake imekamilisha mipango miji kwa
Mji wa Mtwara uendane na mabadiliko ya kiuchumi.
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe alisema
Bandari ya Mtwara haijauzwa na kwamba inapanuliwa ili iweze kukidhi
mahitaji ya baadaye huku akiahidi kufika Mtwara kila baada ya miezi
mitatu ili kutoa taarifa ya maendeleo ya bandari na uwanja wa ndege kwa
wananchi.
“Tulikuwa na eneo la hekta 70 tu za Bandari ya
Mtwara, sasa tumepanua na tunazo hekta 2,994. Tumetenga hekta 110 ili
tuweze kuwa na bandari huru itakayowezesha kuongezeka kwa matumizi,”
alisema Dk. Mwakyembe.
Wenyeji waridhika
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa vyama tisa vya siasa mkoani Mtwara, Uledi Abdallah alisema madai ya wananchi yalikuwa mitambo ya kusafisha gesi ghafi ijengwe Mtwara na kwamba iwapo Serikali imeamua kufanya hivyo madai yao yatakuwa yamekwisha.
“Kama gesi itakayosafirishwa kwenda Dar es Salaam ni ile iliyosafishwa, sisi hatuna tatizo,” alisema Abdallah
Mbunge wa Mtwara Mjini (CCM), Hasnain Murji alimpongeza Waziri Mkuu kwa hatua yake ya kuwasikiliza wananchi na kwamba mzozo huo uliodumu kwa takriban mwezi mmoja sasa umefikia tamati.
Katibu wa Chama cha Wananchi (CUF), Mtwara Mjini, Saidi Kulaga alimpongeza Waziri Mkuu kwa hatua aliyoichukua na kumwomba awaachie huru wale waliokamatwa kutokana na vurugu zilizotokea Mtwara na Masasi ili kujenga mwanzo mpya wa uhusiano baina ya Serikali na wananchi, ombi ambalo Pinda alilipokea na kuahidi kulifanyia kazi ndani ya wiki mbili.
Wataalamu wa gesi
Awali, kutokana na vurugu hizo, zaidi ya wataalamu 50 waliokuwa mkoani Mtwara kwa ajili ya kusimamia mradi wa ujenzi wa bomba la gesi waliondolewa mkoani humo, Mwananchi limebaini.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili jana zilieleza kuwa watalaamu hao wapo Dar es Salaam tangu Jumamosi iliyopita na wamefikia katika Hoteli ya JB Belmont kupisha vurugu za wananchi waliokuwa wakipinga ujenzi wa bomba hilo kutoka mkoani humo kwenda Dar es Salaam.
Mmoja wa viongozi wa hoteli hiyo, ambaye alikataa kutaja jina lake kwa maelezo kuwa si msemaji alikiri kuwapo kwa watalaamu hao katika hoteli hiyo… “Wapo ila walisema kuwa hawa taki kuzungumza na vyombo vya habari.”
Bunge laingilia kati
Spika wa Bunge, Anna Makinda ameunda kamati itakayokwenda Mtwara kuzungumza na kada mbalimbali kuhusu vurugu na mustakabali mzima wa gesi.
Makinda alisema hayo jana muda mfupi kabla ya kuahirisha kikao cha kwanza katika Mkutano wa 10 wa Bunge… “Bunge ni chombo cha amani, tutawatuma wabunge kwenda kuzungumza nao…suala hili linahitaji busara sana.”
Habari hii imeandikwa na Abdallah Bakari (Mtwara), Fidelis Butahe (Dar), Ibrahim Bakari na Habel Chidawali (Dodoma)
MWANANCHI

No comments:
Post a Comment