Mbunge wa Bukoba Mjini (Waziri wa Maliasili na Utalii) Mh. Balozi Hamis Kagasheki
Kwa habari tulizotumiwa na mdau wetu kutoka Bukoba zinesema mgogoro huo kati ya Mbunge wa Bukoba Mjini na pia ni waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Balozi Hamis Kagasheki ameingia kwenye mgogoro na Meya wa Bukoba Mjini Mh. Anathory Amani kwasababu ya suala la ubomoaji wa soko kuu la hapo Bukoba Mjini. Meya wa huyo anashinikiza soko livunjwe na kujengwa la kisasa lakini mbunge wa jimbo ilo na baadhi ya madiwani hawakubaliani na suala hilo kwani hajajulukana hatma ya wafanyabiashara wa soko hilo la Bukoba.
Hili suala lilisababisha madiwani wawili wanaoziwakilisha
kata mbili ndani ya Manispaa ya Bukoba walitembezeana mkono baada
ya kutokea mabishano katika kikao cha maadili chenye lengo la
kumshinikiza Mh. Meya Anathory Amani ajiuzuru.
Madiwani hao
waliopeana kichapo na kuzua taflani kubwa hadi kufikishwa kituo cha
polisi ni Diwani wa Kata ya Kahororo Mh. Chief Kalumuna na Diwani wa
Kata ya Nyanga Mh. Deusdedit Mtakyawa wote wa Chama cha Mapinduzi.
Tukio lililo
endelea ni kupiga kura ya kutokuwa na imani na Meya na inasadikiwa
kutokana na kura zilizopigwa nyingi ni zile zinazo mshinikiza Mh. Amani
kujiuzuru hivyo ndivyo mambo yalivyo.
Pia kesi ya suala la soko kuu la Bukoba iko mahakamani kwani wafanyabiashara wanapinga kubomolewa soko hilo kwani hakuna sehemu ya kuhamishiwa kwa wakati wote wa ujenzi wa soko jipya
HABARI HII NI KWA HISANI YA MDAU WETU WA BUKOBA
No comments:
Post a Comment