Gari la Mh. Edward Lowassa likiwa limebonyea kwa ubavuni baada ya kupata ajali iliyotokea leo asubuhi.
Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa amenusurika
kifo, baada ya gari lake alilokuwa akisafiria kupata ajali eneo la Bwawani mkoani Morogoro.
Gari hilo la Mh. Lowassa liligongwa na basi
la Morobest, wakati basi hilo lilipolipita basi jingine kwenye daraja na
kukutana uso kwa uso na gari lakini dereva wa Mh. Lowasa kwa ustadi
mkubwa alilikwepesha gari lisigonge upande alipokuwa amekaa mzee na
kuligonga ubavuni nyuma kwa upande wa dereva na hakuna
aliyejeruhiwa.
Lowassa na msafara wake aliendelea na safari hadi
morogoro ambako ameshiriki katika harambee ya ujenzi wa kanisa la KKKT Kilakala.
No comments:
Post a Comment