Hii ni mahakama iliyochomwa moto usiku wa kuamkia leo huko Mtwara
Hii ndo Nyumba ya Mbunge
Hawa Gasia iliyovunjwa vioo na kuchomwa moto
Huu nso mwonekano wa Mahakama ya mwanzo iliyochomwa moto usiku wa kuamkia leo
Kwa
kile kinachoaminika kuwa ni kukua kwa mgogoro wa Gesi Mkoani Mtwara na
Kusini kwa ujumla, usiku wa kuamkia leo Mahakama ya Mwanzo katika
Manispaa ya Mtwara Mikindani imeteketezwa kwa moto.
Hivi Serikali iko wapi kutatua Mgogoro wa Gesi ulioingia kwenye taswira Mpya maana sasa tunakoelekea ni kubaya tena sana pia mgogoro huu unasababishwa na Serikali kutowashirikisha wananchi katika maamuzi ya rasilimali zilizoko Tanzania. Kama Serikali isipo tatua mgogoroitapelekea matatizo makubwa kwenye nchi maana kama wananchi wamefikia kuchoma nyumba za viongozi kitakacotokea kama serikali haita tatua mgogoro huu itapelekea watu kupoteza uhai wao kwasababu serikaliimekaa kimya.
Pia kumetokea maandamano yanayo ambatana na vurugu huko Masasi, chanzo kikisemekana kuwa ni kuchoshwa na manyanyaso ya Polisi dhidi ya vijana wa boda boda. Nyumba ya mbunge inasemekana kuharibiwa, na mahakama kuchomwa moto. Baada ya askari wa Masasi kuzidiwa, imebidi waagizwe wengine kutoka Mtwara.
Pia kumetokea maandamano yanayo ambatana na vurugu huko Masasi, chanzo kikisemekana kuwa ni kuchoshwa na manyanyaso ya Polisi dhidi ya vijana wa boda boda. Nyumba ya mbunge inasemekana kuharibiwa, na mahakama kuchomwa moto. Baada ya askari wa Masasi kuzidiwa, imebidi waagizwe wengine kutoka Mtwara.
Taarifa za
redio tulizozipata kwasasa ni kwamba wananchi wanaendelea kufanya uharibifu
mkubwa huko ambapo naambiwa wamevamia gereza wakafungulia wafungwa na
kisha kupiga moto gereza. Polisi wamezidiwa na wamejifungia kituoni
wanarusha mabomu yao tokea huko walikojificha maana nje hakutamaniki. Na pia
wameshateketeza nyumba ya mama Anna Abdallah.
Wito wangu kwa Serikali ni kuwa, muda huu ni kukaa na
wananchi ili kujadiliana juu ya mstakabali mzima wa tatizo hili na
kutafuta suluhu juu ya suala la Gesi na pia Maasikari wasitumie nguvu kupita kiasi.
''Mungu ilinde Tanzania tusifike huko tunakotaka kufika''
No comments:
Post a Comment