Kijana Dickson Vedastus
Kijana
mmoja Dickson Vedastus Mkazi mmoja wa Kirumba Mkoani Mwanza amewaomba
watanzania kumchangia shilingi milioni 25 ili akatibiwe maradhi ya
kibofu cha mkojo yanayombumbua kwa miaka kumi na saba sasa.
Kijana
huyo ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari
ya Kirumba amesema fedha hizo zitamsadia kwenda nchini India kwa ajili
ya matibabu ambayo yameshindikana hapa nchini.
Kijana
huyo amewahi kupatiwa matibabu katika hospitali mbalimbali hapa nchini
bila mafanikio na ndipo madaktari wakamshauri kwenda nchini india kwa
matibabu zaidi kutokana na ukubwa wa tatizo la maradhi yanayomsumbua.
Kwa
yeyote ambaye ameguswa na maradhi ya kibofu cha mkojo yanayomkabili
Dickson anaweza kuwasiliana naye kwa simu nambari 0762 32 45 27/0683 58
00 04.
Picha na Amicus Butunga, TBC Mwanza.
No comments:
Post a Comment