Kuna maandamano yamefanywa na wananchi eneo la Dumila. Chanzo ni mgogoro kati ya WAKULIMA na WAFUGAJI. Makazi ya wafugaji yamechomwa moto. Mpambano unaendelea wananchi wamebeba silaha za jadi wanaelekea kituo cha POLISI.Wananchi wakulima wanamtaka Mkuu wa Mkoa wa Morogoro (Joel Bendera) kufika kuwatatulia tatizo lao la kunyang'anywa maeneo yao na kuwapatia wafugaji.
Wananchi hao wamegawanyika katika makundi kadhaa huku kila kundi
likifunga barabara ya kuingia na kutoka eneo hilo la Dumila, ambapo
wamezuia magari yote yanayopita eneo hilo kutoka Morogoro na kutoka
Dodoma.
Tayari Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, ameomba udhuru kutoka katika Kikao cha
wakuu wa mikoa, kilichokuwa kikiendelea mkoani Dodoma na yupo njiani
akielekea eneo hilo kwa nia ya kukutana na wananchi hao ili kuwasikiliza
na kutatua mgogoro huo
Wafugaji wanapendelewa na mkuu wa wilaya na mapolisi kwa kuwa wanahonga sana.
Mgogoro wa eneo hilo na wilaya ya Kilosa kwa ujumla ni mkubwa sana na wa miaka mingi sana (Nilishawahi kufanya research huko 2003 kuhusu migogoro ya ardhi). Inashindikana kutatuliwa kwa kuwa wafugaji wana uwezo wa kuhonga wakati wakulima hawana uwezo wa kuhonga.
Kumbukeni mgogoro wa Msovero mwaka 2001 ambako watu zaidi ya 100 walikufa. Serikali ya CCM imekuwa ikumbatia hii migogoro bila kutafuta suluhisho la kudumu. Pia mapendekezo ya sheria ya ardhi ambayo yangemaliza kabisa migogoro hii ya wakulima na wafugaji yalikataliwa na wabunge wanaotokea maeneo ya wafugaji kwa kuwa ingewanyima haki ya kugeuza nchi nzima eneo la malisho.
Serikali ya CCM imeshindwa kuleta maendeleo na inashindwa hata kutatua migogoro ya ardhi. Shime watanzania tuikatae CCM.
JAMII FORUMS
No comments:
Post a Comment