HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » FFU wa Ngoma Africa band wapo kambini kujiandaa na vita vya "kuziba Nyufa"

Ngoma africa live in frankfurt 
 
FFU wakiwa na mitutu yao
 
 Hii ni cover ya CD  kwa upande wa mbele.
Hii ni cover ya CD kwa nyuma.
FFU nao kuingia kambini.

FFU wa Ngoma Africa Band wapo kambini ! msituni! Watangaza Vita Mpya ya "KUZIBA NYUFA" katika mpasuko wa Jamii!
  Habari za uhakika tena nyeti zimevuja kutoka katika kambi ya bendi  maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band" aka FFU yenye makazi  yake nchini Ujerumani. Kuwa bendi hiyo inayofanananishwa na kikosi kazi FFU imeingia kambini katika msimu  wa barafu huko ughaibuni, kwa kujifua na kujiandaa kwa kuwaletea washabiki vitu vipya ! Pia
Kiongozi wa bendi hiyo Kamanda Ras Makunja mwanamuziki mwenye mjina mengi ya kutisha tisha kama vile kamanda wa FFU, Kolokoloni namba 1,mfalme Hui Hui wa gagagigikoko n.k, kamanda alikaririwa mwanzoni mwa Januari 2013 kuwa Bendi hiyo inaenda kambini Kujiandaa na vita ! alipoulizwa vita gani? alijibu vita vipya vya
"KUZIBA NYUFA" zilezojitokeza katika jamii yetu!
Ndio kusema Kamanda wetu wa FFU Ras Makunja kaingia kambini na kikosi
chake kujiandaa na vita? vita venyewe vya kuziba nyufa na mimomonyoko au mipasuko katika jamii yetu! kauli ya kamanda Ras Makunja inaonekana inadarubini ya mtazamo mkali unaoona mbali! katika mahojiano na jarida la africa analysis la Uingereza, Ni siku chache tu bendi hiyo yenye tabia za ki-FFU ilionekana katika
  uwanja wa ndege wa Bremen,wakiwa wanaondoka lakini wakusema wapi wanako elekea, "wanamuziki wa bendi hiyo wakiwa na mizigo" nyusoni wakiwa seriously tena  hawakuwa tayari kujibu chochote wanachoulizwa ! tena katika msimu wa baridi na barafu wanaenda kambini? tena haijulikani nchi gani?
kama Serbia au Bosnia ? pengine Israel ! hakuna anayejua !

Kamanda Ras Makunja na ffu wa Ngoma Africa Band wapo kambini,kwa
  kujiandaa na vita vya kuziba nyufa, na mwaka huu pia bendi hiyo inatimiza miaka 20 tangu izaliwe mwaka
1993 hadi mwaka huu 2013 ni umri mkubwa. Washabiki wanasubiri kwa hamu kubwa kuona na kujiunga na na vita
  vilivyotangazwa na bendi hiyo chini ya kamanda Ras Makunja mwenye kichwa kigumu au mkuu wa "Watoto wa Mbwa" Ngoma
Africa.


PICHA KWA HISANI YA MSEMA KWELI

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: