Na John Banda, Dodoma
MAMLAKA ya maji safi na maji taka mjini
Dodoma [DUWASA] wameitaka mamlaka ya
ustawishaji makao makuu CDA kuwa makini katika utendaji wake wa kazi ili
kuepuka hasara zisizo za lazima huku wakiwasababishia wananchi kuishi kwa
taharuki kutokana na kukumbushwa wapendwa wao waliokufa miaka mingi iliyopita.
Hayo yalisemwa na Msimamizi wa uunganishaji
maji Abdalla Gwanguzo wakati wananchi wa Ilazo
walipokuwa wakichimba kaburi na kurudishia masalia ya marehemu yaliyochimbuliwa
na mafundi wa DUWASA walipokuwa wakichimba Mitaro wa kupitishia bomba kwenda
kwa mteja wao.
Gwanguzo alisema wao DUWASA hawana kosa
lolote kuhusu uhalibifu huo wa kaburi la watu isipokuwa CDA ndiyo waliokosea
kuwapa watu maeneo hayo ili wajenge na huku wakijua watahitaji na huduma kama
hizi za maji na hata umeme bila kuwauliza wenyeji waliowahi kuishi maeneo haya
ili waseme kama kuna vitu hivi., mafundi wasingeweza kujua bila kuelekezwa.
‘’DUWASA tumetoa kiasi cha Tsh. 271,000 na
kuwanununlia sanda, mfuko wa nailoni na gharama za kuhifadhi mabaki Marehemu
Chaguna iliyofikia kiasi cha laki tatu 300,000 kuhusu garama za kuhamisha
kaburi ni jukumu la CDA”, alisema
Kwa upande wake mjukuu wa Marehemu hao
waliozikwa maeneo hayo Emilia Joshua 56
aliwataja kuwa ni Babu na Bibi zake
Chihuna na Nhondolwa Mgazwa waliozikwa zaidi ya miaka 50 iliyopita
katika eneo hilo la ilazo zamani
lilijulikana kwa jina la Sanguti alisema alihama eneo hilo miaka ya 1972 na
kuhamia kijiji jirani cha nzuguni.
Joshua alisema alipata taarifa kutoka kwa wapita
njia waliokuwawakipita njia katika eneo hilo kwamba waliona kaburi moja
limechimbuliwa ndipo alipofika na kukuta hali hiyo akaenda kutoa taarifa kwa
mwenyekiti wa mtaa.
‘’Ni vizuri wakiwa wanatuambia mapema kama wanataka kufanya chochote ili tuwe
tunatoa maelekezo maana eneo hili
lilikuwa la kutambika kwanini wanatuonea sijui kwasababu ya unyonge wetu au
umasikini ndiyo maana wanawapa matajili maeneo yetu kwa ubabe basi watuhamishie
tujue moja kuliko kudhalilisha mifupa ya ndugu zetu,’’ alisema mjukuu huyo
Mwenyekiti wa Mtaa huo Denis Mwaluko
Chimalusotola alisema alipata taarifa hiyo na kuwasiriana na afsa afya wa kata
na ndipo hatua zingine zikafuata na kufikia hatua hiyo na kuishauri CDA
kuhakikisha wanawafanyia wananchi vizuri kwani hayo ni maeneo yao ya asili
hivyo ni vizuri wawajulishe mapema
kuhusu wanachotaka kufanya.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamraka ya ustawishiji
makao makuu [CDA] Ibrahim Ngwada alipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusiana na mkakanganyiko huo
alisema wanautaratibu wa kutoa fidia na kuhamisha masalia ya marehemu waliokuwa
wamezikwa maaneo yaliyopitiwa na mradi mpya kama huo wa kupitisha mitaro ya
maji na kuyapeleka eneo lililotengwa kwa ajili ya makaburi.
‘’Mamraka haiwezi kujua kwamba mahali gani
palikuwa na nini kutokana na maeneo yenyewe kutokuwa na alama za kuonyesha kama
kulikuwa na makaburi, hivyo ni jukumu la wananchi wenyewe kuorodhesha na
kutuonyesha maeneo yenye makaburi ili tuwape fidia na kuyahamisha kabla ya
ujenzi wowote kuanza’’, aliseama
Mwishoni mwa mwaka uliopita Tukio kama hilo
lilijitokeza katikamradi wa Njedengwa ambapo kampuni ya uchimbaji ili kutandikamabomba
ya maji safi na maji taka ambapo Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya ustawishaji makoa makuu [CDA]
Pascus Mulagiri aliwahi kusimamisha kazi
ya uchimbaji isiendelee mpaka watakapolipa fidia na kuhamisha makaburi
yaliyokuwepo Eneo la Mradi.
HABARI KWA HISANI YA JOHN BANDA
No comments:
Post a Comment