RAIS JAKAYA KIKWETE AZINDUA UGAWAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akibonyesha kitufe kuashiaria kuzindua rasmi mfumo wa usajili na utambuzi wa watu na utoaji wa vitambulisho vya taifa uliofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.Watatu kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dkt.Emmanuel Nchimbi, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Bwana Mwaimu na kulia nia Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bwan Said Meck Sadik.
  
Rais Dk.Jakaya Kikwete na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiangalia bango lenye Kitambulisho cha Taifa cha Rais Kikwete muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuzindua mfumo wa usajili na utambuzi wa watu na utoaji wa vitambulisho vya taifa uliofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaamn jana. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk.Emmanuel Nchimbi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt.Emmanuel Nchimbi akimkabidhi mke wa Rais Mama Salma Kikwete kitambulisho chake cha Taifa katika viwanja vya Karimjee leo huku Rais Kikwete akishuhudia,kushoto Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Bwana Mwaimu.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa kitambulkisho cha taifa katika viwanja vya Karimjee leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rais Mstaafu awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi kitambulisho chake cha taifa katika viwanja vya Karimjee leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rais Mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume kitambulisho chake cha taifa katika viwanja vya Karimjee leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad kitambilisho cha Taifa katika viwanja vya Karimjee leo wakati wa hafla ya Uzinduzi wa mfumo wa usajili na utambuzi wa watu.
 Rais Kikwete akimkabidhi Kada wa CCM Mzee Kingunge Ngombale Mwiru kitambulisho cha taifa.
 Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Alex Malasusa kitambulisho chake cha taifa.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Shekhe Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Alhaj Elihad kitambulkisho cha taifa
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Mwenyekiti wa CUF Professa Ibrahim Lipumba kitambukisho cha taifa.
 Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt.Ramadhani Dau kitambulisho cha taifa leo katika viwanja vya Karimjee.
Rais Dkt.Jakaya Kikwete akimkabidhi mkurugenzi Mkuu wa PPF Bwana William Eriyo kitambulisho cha taifa
 
PICHA KWA HISANI YA FREDDY MARO

No comments

Powered by Blogger.