TUNDA la stafeli linatibu magonjwa kadhaa,
ikiwamo saratani kwa ubora wa karibu mara 10,000 ya matibabu ya kawaida
yanayopatikana kwenye vituo vya afya, utafiti umebaini.
Utafiti huo uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Dawa
cha Purdue nchini Marekani, umeeleza kuwa mbali na kutibu saratani,
tunda hilo pia ni tiba ya matatizo ya msongo na mfadhaiko.
“Maajabu ya stafeli ni kwamba lina uwezo wa
kuangamiza chembehai zenye saratani pasipo kusababisha madhara katika
mwili kama zinavyofanya dawa nyingine za ugonjwa huo au mionzi,” imesema
sehemu ya utafiti huo uliochapishwa kwa mara ya kwanza katika Jarida la
Kemia na Madawa la nchini Marekani, mwaka 2010.
Taasisi ya utafiti wa Saratani ya Nchini Uingereza(NIR) ilifanya utafiti wa kwanza kuhusu maajabu ya stafeli mwaka 1976.
Katika utafiti huo ilibainika kuwa majani, mizizi
na tunda la stafeli, vina uwezo wa kutibu saratani, lakini matokeo ya
utafiti huo hayakutangazwa kwa umma kwa hofu ya kuua viwanda vya dawa za
saratani.
Inaelezwa kuwa kirutubisho kilichopo katika
stafeli kinatumia jina la kibiashara la ‘Triamazon’ na kimepigwa
marufuku kutumika nchini Uingereza na Marekani kutokana na uwezo wake
mkubwa wa kitiba.
Utafiti mwingine uliofanywa na Chuo Kikuu cha
Kikatoliki nchini Korea na kuchapishwa katika jarida la Bidhaa Asilia
ulibaini kuwa stafeli lina uwezo wa kuponya saratani ya tumbo.
Utafiti wa chuo hicho ulienda mbali na kusema kuwa
tunda hilo linaweza kulenga seli za saratani tu, bila kushambulia seli
muhimu za mwili kama ambavyo tiba ya mionzi ifanyavyo.
Tunda la Stafeli lina kirutubisho muhimu kiitwacho
Annona Muricata, ambacho ndicho chenye uwezo wa kupigana na maradhi ya
saratani.
Imeelezwa kuwa stafeli lina uwezo wa kutibu aina 12 za saratani ikiwemo ya matiti, kongosho, mapafu na ya kibofu cha mkojo.
Pamoja na kutibu saratani, kirutubisho hicho
kilichopo katika tunda hilo pia huweza kutibu vimelea, shinikizo la
damu, msongo wa mawazo, matatizo ya mfumo wa fahamu na sukari.
Utafiti huo unaonyesha kuwa kirutubisho
kimegwacho katika tunda hilo kinaweza kwa asilimia kubwa kupambana na
saratani bila kumuacha mgonjwa na madhara kama kusikia kichefuchefu,
kutapika, kupungua uzito na kunyonyoka nywele.
Aidha huweza kuupa mwili kinga na kukupa nguvu bila madhara yasababishwayo na dawa nyingine.
Tangu mwaka 1976, tunda hilo liliendelea kufanyiwa utafiti katika maabara binafsi zaidi ya 20duniani.
Tangu mwaka 1976, tunda hilo liliendelea kufanyiwa utafiti katika maabara binafsi zaidi ya 20duniani.
Stafeli nini?
Stafeli ni tunda la chanikiwiti ambalo linastawi zaidi katika ukanda wa kitropiki.
Stafeli ni tunda la chanikiwiti ambalo linastawi zaidi katika ukanda wa kitropiki.
Mti wa tunda hilo ni mfupi wa wastani, Wabrazili
wanauita Graviola na Waingereza wanaliita Soursop. Hapa Tanzani stafeli
linajulikana kwa jina jingine la topetope.
Kwa Waingereza, tunda hili ni kubwa lenye uchachu
wa kati na utamu mwingi. Ndani yake kuna maganda yenye weupe kama sufi
na limesheheni juisi.
Mkurugenzi wa Utafiti wa Taasisi ya Utafiti wa
Tiba (NIMR) Dk Julius Massaga, alisema taasisi yake haijawahi kufanya
tafiti ya aina yoyote kuhusu tiba ya saratani.
“Tuna kitengo cha masuala ya tiba na mambo mengine
lakini hatujawahi kufanyia utafiti tunda la stafeli wala dawa nyingine
yoyote ya saratani,” alisema Dk Massaga
Mtaalamu wa masuala ya tiba za vyakula, Boniphas
Sosthenes wa kituo cha Tiba cha Neema, jijini Dar es Salaam, alisema
anafahamu uwezo huo wa stafeli kutibu saratani, lakini hajathibitisha
kitalaamu.
Daktari aliyewahi kumtibu Baba wa Taifa Mwalimu
Julius Nyerere, Dk Keisy Mtambo alisema taarifa za kuwa stafeli linaweza
kutibu saratani anazisikia, lakini hana uhakika
“Nasema sina hakika kwa sababu satani ina hatua mbalimbali na kwa watu tofauti,” alisema.
Alisema kwa anavyoifahamu saratani, ni vigumu mno
kutibika kwa tunda tu, labda kama tunda hilo limefanyiwa kazi za
kitabibu zaidi.
“Kuna saratani kwa watoto, wazee na watu wenye VVU, zina utofauti mkubwa na utafiti huo haujaeleza bayana,” anasema
MWANANCHI
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment