Mwenyekiti wa kamati ya TWAA Bi Sadaka Gandi akiongea na Waandishi wa Habari Leo
DAR ES SALAAM, TANZANIA, – Taasisi ya Tanzania Women of Achievement (TWAA) imezindua Tuzo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania msimu wa 2013 zilizopangwa kufanyika katika siku ya wanawake duniani tarehe 8 Mwezi Machi mwaka huu. Tuzo hizi ambazo hufanyika kila baada ya miaka miwili zilizinduliwa mwaka 2009 kwa heshima ya wanawake katika sekta mbalimbali nchini kote ambao kupitia kazi zao wamechangia kwa kiasi kikubwa sana kuleta maendeleo ya jamii zao kwa njia moja au nyingine.
DAR ES SALAAM, TANZANIA, – Taasisi ya Tanzania Women of Achievement (TWAA) imezindua Tuzo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania msimu wa 2013 zilizopangwa kufanyika katika siku ya wanawake duniani tarehe 8 Mwezi Machi mwaka huu. Tuzo hizi ambazo hufanyika kila baada ya miaka miwili zilizinduliwa mwaka 2009 kwa heshima ya wanawake katika sekta mbalimbali nchini kote ambao kupitia kazi zao wamechangia kwa kiasi kikubwa sana kuleta maendeleo ya jamii zao kwa njia moja au nyingine.
"TWAA inataka kutambua wanawake,
waishio Tanzania ambao kupitia kazi zao wameweza kupata mafanikio
makubwa sit u kibinasi bali wametumia nafasi zao kuleta maendeleo na
mabadiliko ya kimsingi kwenye jamii zinazowazunguka." Alisema Mkurugenzi
mkuu wa TWA Bi. Irene Kiwia. "Tuzo hizi mbazo sasa ziko katika msimu
wake wa 3 zinatoa fursa nzuri ya kutambua na kupongeza wanawake ambao
wamechangia sana kwenye kubadilisha na kuboresha sura ya Tanzania. Kwa
wanawake wengi hii itakuwa mara ya kwanza mafanikio na michango yao
imetunukiwa na hili ni jambo la kufajiri na kuridhisha sana.”
Vipengele vya tuzo za mwaka huu ni
Sanaa na Utamaduni, Biashara na Ujasiriamali, Habari na Mawasiliano,
Michezo, Professional (Kazi), Elimu, Afya, Ustawi wa Jamii, Sayansi na
Teknolojia, Sekta ya Umma, Kilimo na Mshiriko Mdogo.
Bi Sadaka Gandi, mwenyekiti wa kamati
ya TWAA alitoa wito kuwa "tunawasihi mashirika, vyama, wanawake na
wanaume kote Tanzania kuteua wanawake wenye mafanikio katika makundi
haya na kuonyesha mchango wao katika uwezeshaji wa wanawake. Kuna maelfu
ya wanawake wastahili wa tuzo hizi huko nje ambao ni mawakala wa
mabadiliko katika jamii zao. Tunataka kuimba mapambio ya mashujaa hawa
na kuhamasisha mamilioni ya wanawake wengine wa Tanzania kuiga mifano na
kupata msukumo wa kuleta mabadiliko. Kamati ilipokea fomu za nyingi
sana za washiriki miaka ya nyuma na hivyo basi tunategemea ushiriki
mzuri zaidi mwaka huu. "
Kamati ya TWAA inawajumuisha Bi Mary
Rusimbi - Mwanaharakati na Mwanzilishi wa Programu ya Mtandao wa Jinsia
Tanzania, Jaji Joaquine De Mello - Kamishna wa Tume ya
Haki za Binadamu
na Utawala Bora, Dk Marcelina Chijoriga- Mkurugenzi kutoka Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam, Bi. Ludovicka Tarimo – Mtaalamu wa Jinsia kutoka
USAID, Bwana. Innocent Mungy-Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka Mamlaka ya
Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), Sadaka Gandi - Mwanasaikolojia
na mfanyakazi za Jamii, Irene Kiwia - Mwanzilishi na Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya mahusiano ya jamii Frontline Porter Novelli. Huko
nyuma tuzo hizi zilidhaminiwa na Baileys, Delloite, NBC, Home Shopping
Center, TCRA, Songas, Watu wa Marekani, DTP, UN DPG Gender Group, UNFPA,
UNESCO, TBL, Multichoice, African Life Assurance, Barrick, Twiga
Cement, Vodacom, Farm Equip, RBP, Clouds FM na Frontline Porter Novelli.
KUHUSU TANZANIA WOMEN OF ACHIEVEMENT (TWA)
TWA ni taasisi isiyo ya kiserikali,
ya hiari na kujitegemea inayojihusisha na uwezeshaji wa wanawake
iliyoanzishwa mwaka 2009. Lengo kuu la TWA ni kuimarisha ushiriki, na
majukumu ya wanawake na uwezo wao katika jamii ya Tanzania kwenye mabo
ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. TWA inafanya kampeni,
mafunzo, semina, mikutano na warsha ambazo zinakuza ubadilishanaji wa
taarifa na ushauri kwa wanawake na wasichana wadogo wa Kitanzania.
Kampeni na mafunzo haya yanalenga
zaidi haki za binadamu na za wanawake, usawa wa kijinsia, ushiriki wa
wanawake kweye shughuli za kiuchumi na kijamii.Kazi kubwa ya TWA ni
kuboresha maisha, kupanua fursa, na kuwasaidia wanawake katika Tanzania
kushamiri na kuchangia kwenye ustawi wa nchi. TWA inafanya kazi na
viongozi ,watu binafsi, jamii, mashirika yasiyo ya kiserekali, serikali,
sekta binafsi na wafadhili wa nje kujenga ufanisi na kuhakikisha
malengo ya kuendeleza wanawake yanafanikiwa. Sisi ni kosa kwa maendeleo
ya Tanzania kuendelea mpaka kila mwanamke anakuwa mabadiliko. Tumejikita
kuhakikisha kuwa Tanzania inaendelea na wanawake ni chachu ya maendeleo
hayo.
MJENGWA
No comments:
Post a Comment