Dereva wa Lori
la Maji wa Kampuni ya Dolfin yenye maskani yake Mbezi Tang Bovu, jijini
Dar es Salaam,ambaye hakuweza kufahamika jina lake mapema, akiugulia
maumivu baada ya kupigwa na kuumizwa na jamaa wawili waliokuwa na kina
dada wawili katika gari ndogo eneo la Mbezi njia inayoingia katika Shule
ya Mbezi Beach Sekondari jana usiku.
Dereva
huyu alikuwa akitokea Barabara kubwa akiingia katika njia ndogo
inayoelekea Shule ya Sekondari ya Mbezi Beach, na gari ndogo ilikuwa
ikitokea katika njia hiyo ndogo na kukutana uso kwa uso na lori hilo,
huku watu waliokuwa katika gari hiyo ndogo wakimtaka dereva wa lori
kuwapisha wao ili waanze kupita.
Dereva
huyu aliamua kubana kushoto na kuwaachia njia ili wapite, kama picha ya
Lori inavyoonyesha chini, laiki jamaa waliokuwa katika gari ndogo
waliamua kushuka na kumshusha dereva huyo na kisha kuanza kumshambulia
kwa magumi na mawe, huku dereva huyo akitoka nduki na kuacha gari lake,
hadi katikati ya barabara inayoelekea Tegeta ikitokea Mwenge, walipomtia
mikonini na kuanza kumpiga kama mwizi huku wakitumia mawe kumpigia kama
makwenzi, na kumuumiza kama hivi, hadi walipofika watu kibao na kuanza
kuamulizia ugomvi huku wakijua kuwa jamaa huyo ni mwizi huku wengine
wakijandaa kuanza kumshambulia.
Lakini
watu hao baada ya kupata stoti kamili ilivyokuwa waliamua kuwageuzia
kibao watu hao wakianza kuwasonga kutaka kuwashambulia ndipo walipoamua
kudandia gari na kukimbia, huku mmoja kati ya wanawake waliokuwa na
jamaa hao, akisikika kumwambia jamaa huyo,
''usirudie kutukana watu waliovaa suti hovyo bila kuwajua watakuua''.
Gari
hiyo wakati ikianza kuondoka eneo hilo hukuikiendeshwa na mwanamama,
ilianza kushambuliwa kwa mawe kwa bahati iliwahi kuondoka eneo hilo na
kuingia usawa wa Barabara ya Masana na kutokomea.
Watu hao wakidandia gari iliyoanza kutembea ili kutoweka eneo hilo.
Jamaa hao wakianza kuondoka eneo hilo kwa kasi huku gari hiyo ikiendeshwa na Mwanamama.
Lori
lililozua kasheshe hilo, ndiyo hili na eneo lenyewe ndo kama hivi
linavyoonekana huku magari yakiwa na uwezo wa kupita bila kugusana na
lori hilo.
Lori
hilo likiwa limeachwa katika eneo la tukio baada ya dereva wake kupewa
kipondo huku magari mengine yakipita kama kawaida.Picha na Sufiani
Mafoto Blog.
No comments:
Post a Comment