MOJA YA MTOTO MAJERUHI AKIHAMISHWA KUTOKA KATIKA HOSPITALI YA MISION CHIMARA NA KUPELEKWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA |
MOJA YA MAJERUHI AKISUBIRI KUPATA MATIBABU
HILI NDILO ROLI WALIMOPANDA VIBARUA HAO WA SHAMBA LA KAPUNGA
KWELI MUNGU NI MKUU HUWALINDA WATOTO WADOGO HAPA MKUU WA MKOA AKIMPA MOJA YA WATOTO WALIOPATA AJALI
HUYU BINTI NI MWANAFUNZI NAE ALIKUWEPO KWENYE AJALI HIYO
MKUU WA MKOA MBEYA ABAS KANDORO AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI
HAWA WOTE NI WANAFUNZI WALIKUWA WANAENDA KUFANYA KIBARUA CHA KULIMA KWA MWEKEZAJI KATIKA SHAMBA HILO LA KAPUNGA
MAJERUHI WAKISAFIRISHWA KWENDA MBEYA
WATU watano wamepoteza maisha na
wengine 130 wamejuruhiwa vibaya huku hali zao zikiwa mbaya baada ya Lori
walilokuwa wakisafiria shambani kuacha njia na kupinduka katika kijiji cha
Mapogolo kata ya Itamboleo Wilayani Mbarali Mkoani hapa.
Ajali hiyo imetokea leo saa 1:30
asubuhi ambapo lori hilo ambalo ni mali ya Mwekezaji wa shamba la Kapunga
Rice Project, na kwamba watu hao walikuwa wakielekea kwenye shamba la mwekezaji
huyo lililkuwa limebeba vibarua hao zaidi ya 200 ambao ni wakazi kitongoji cha
Kapunga.
Lori
hilo
lenye namba za uasjili T398 BSE Scania Tipa, ambalo lilikuwa
likiendeshwa na
dereva aliyejulikana kwa jina Baraka Moreli, lilionekana likiwa katika
mwendo kasi na dereva huyo akiwa na lengo la kutaka kuipita
pikipiki iliyokuwa mbele yake. huku akishangiliwa na vibarua hao ipite
ipite hiyo pikipiki haiwezi kutushinda sisi gari kubwa moja ya majeruhi
alisema. ndipo walipofika kwenye kona dereva lilimshinda gari hilo na
kupinduka
Akiwa Hospitalini hapo Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro ambaye aliweza kufika hospitalini hapo alisema
kuwa mara baada ya kupata taarifa ya ajali hiyo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya
,Mbarali Gullam Hussein Kiffuu, huku akiombwa kupatiwa msaada wa kuongezewa
madaktari, kuongezewa vifaa vya mataibu sambamba na uwezekano wa kupata damu
kwa ajili ya kuwaongezea majeruhi hao alifanikiwa kuwasiliana na uongozi wa
hospitali ya Rufaa ya Mbeya, hospitali ya Mkoa ili kuweza kuona namna ya kwenda
kuokoa maisha watanzania hao.
Kandoro, alisema kuwa
katika ajali hiyo wanaume wanne wamefariki na mwanamke mmoja. watatu wametambuliwa Samweli Mapugilo mbena 30 mkazi wa Ilembula Bon Mfupa 27 mkazi wa mapogolo na Edgar Mwakipesile 35 mkazi wa Nonde Mbeya. Aidha, Kandoro alisema kuwa idadi ya majeruhi katika ajali hiyo kuwa ni 130 ambapo wanawake ni 40 na
wanaume 89 huku idadi ya watoto waliokuwa wameongozana na wazazi
wao haikuweza
kufahamika kwa haraka.
PICHA KWA HISANI YA MBEYA YETU
No comments:
Post a Comment