Wananchi wakiwa wameubeba mwili wa mtoto huyo baada ya kutupwa
Na Zuhura Zukheli
MTOTO anayekadiliwa kuwa wa mimba ya miezi sita amekutwa amefariki
dunia baada ya kutupwa na mtu asiyefahamika
Tukuio hilo limetokea leo majira ya saa 7:30 mchana katika
eneo la shule ya msingi ya Mtwivila manispaa ya Iringa.
Mashuhuda watukio hilo wamesema kuwa tukio hilo ni lapili
kutokea katika kata hiyo wakati tukio lingine lilitokea wiki mbili zilizopita “haya
matukio tumechoka nayo wanawake wamekuwa wauwaji hawana hata hofu ya mungu
tukio hili jamani sio lakwanza wikimbili zilizopita tumokota mtoto katika kata
hii kwanini wanashika mimba kama hawajajipanga”alisema Rukia Juma.
Naye Edina Coster alisema kuwa kitendo chakutupa watoto
kinasikitisha ndani ya mkoa wa Iringa kwakuwa sasa imekuwa kama mchezo”kama
hivi leo ametupa mtoto huyu wakiume ambae huenda angekuwa kiongozi wa dini au
wa serikali inauma sana” alisma.
Kwa upande wake Zakaria Mufuga alisema kuwa ugumu wa maisha
na kutojipanga kwa katika uzazi imekuwa ni sababu kubwa ya watoto kutupwa” hili
tatizo la kuendekeza ugumu wa maisha ndio sababu ya watu kugeuka wa uwaji
unakuta mtu asnspenda starehe lakini kupanga uzazi hawezi matokeo yake anashika
mimba isiyo tarajiwa anatupa mtoto huu ni ukatili mkubwa”alisema
“Watu wanatafuta watoto kwa hospitali na kwa waganga wa jadi
hawapati dada zetu mnapata mimba mnatoa hivi kwanini msifunge tu vizazi muwe
huru” alisema Emmanuel Msungu.
Mmoja wa wazazi Charles Sia aliyebeba kiumbe kwenda
kukistiri alisema kuwa wazazi wanachangia tatizo la utupwaji kwa watoto
kutokana nakutokuwa na upendo katika na familia zao”wazazi tupunguze ukatili
kwa watoto wazazi tumekuwa wakali kiasi ambacho mtoto anapata ujauzito anaogopa
kusema na matokeo yake wanatoa mimba nakuwatupa watoto kama takataka
Mzazi mwingine aliyeshindwa kuzuia machozi yake alisema kuwa
wazazi wanapata tabu kuwalea halafu wao wanageuka kuwa makatili na kuwatupa
watoo”wanaotupa watoto hatuwataki sisi tunapata tabusana kuwalea kwanini
mnatupa watoto.
Mzee huyo alimalizia kwa kwi kwi ya kulia na kusema kuwa mungu
amuweke mahala pema mtoto huyo kwa kuwa ni malaika ambaye hajamkoesa mtu.
No comments:
Post a Comment