Dimba la Wembley dakika chache kabla ya
kuanza kwa mtifuano wa fainali ya Mabingwa Ulaya kati ya Bayern Munich
na Borussia Dortmund zote za Ujerumani.
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel (wa
pili kulia), akiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza kwa mtanange huo wa
fainali kwenye Uwanja wa Wembley jana usiku.
Mshambuliaji wa Timu ya Buyern Munich, Arjen Robben, (katikati) Thomas Mueller (kushoto) na Franck
Ribery, wakishangilia kwa pamoja bao la Robben, alilifunga kipindi cha
pili wakati wa mchezo wa Fainali wa Ligi ya Mabingwa kati yao na Borussia
Dortmund, uliochezwa usiku huu kwenye Uwanja wa Wembley. Katika mchezo
huo Buyern wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kutwaa Kombe hilo.
Kipa wa Bayern, Manuel Neuer, akizuia shuti la mchezaji wa Dortmund, Robert Lewandowski (kushoto)
Mshambuliaji wa Buyern Munich, Mario Mandzukic, (kulia) akifunga bao.
Arjen Robben akidhibitiwa na wachezaji wa Borussia Dortmund's Neven Subotic na Lukasz Piszczek (kulia)
Arjen Robben (kushoto) na Mario Mandzukic, wakishangilia.
Mchezaji wa Buyern Munich, Franck Ribery (kulia) akiruka kwanja................
Arjen Robben (katikati) akimchambua Kipa wa Dortmund, Roman Weidenfeller na kufunga bao la pili, wakati wa Fainali hiyo.
Nahodha wa FC Bayern Munich ya
Ujerumani, Phillip Lahm akiwa ameshikilia taji la Ligi ya Mabingwa
Ulaya, walilolitwaa jana usiku baada ya kuichapa Borussia Dortmund pia
ya Ujerumani kwa mabao 2-1 katika fainali iliyopigwa kwenye dimba la
Wembley jijini London.
Wachezaji wa Bayern Munich wakiendelea kushangilia ubingwa huo.
No comments:
Post a Comment