Lundenga , Miss Tanzania Brigitte wawafunda Redds Miss Kibaha 2013

Na Mwandishi Wetu

KAMATI ya Miss Tanzania ikiongozwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya International Agency ikiongozwa na Mkurugenzi wake pia Mratibu Hashim Lundenga imewafunda ipasavyo warembo wanaoshiriki katika shindano la Redds Miss Kibaha 2013 litakalofanyika Mei 17 katika ukumbi wa Container mailimoja Kibaha.

Akizungumza wakati alipowatembelea katika kambi yao warembo hao Lundenga aliwataka washiriki hao wajijengee hali ya kujiamini na kila mshiriki asimwogepe mshiriki mwenzake huku akiwataka kila mmoja awe amejiwekea lengo la kufika katika shindano la Kanda na hatimaye taifa.

Aidha Lundenga amewaasa warembo hao kumpa sapoti mrembo atakayetwaa taji hilo ,” endapo mrembo mwenzenu yeyote ataiobuka na kutwaa taji lazima mumpe sapoti kubwa kwani ‘crown’ huvaliwa na mrembo mmoja tu hivyo nawatakia kila la kheri katika shindano lenu na niwaahidi tutakuwa pamoja hadi siku ya shindano”alisema Lundenga.

Mwisho Lundenda alimazia kwa kusema kuwa mrembo atakayeonesha utovu wa nidhamu atatolewa katika shindano hata kama itakuwa ni siku ya fainali hivyo amewataka wawe makini wakati wote.

Wakati huohuo Miss Tanzania 2012 Brigite Alfred aliyeambatana na kamati hiyo alitumia fursa hiyo kutowa mashaka ya mrembo kupangwa kuanzia katika ngazi ya awali hadi taifa.

“Warembo wenzangu kwanza nawapongeza kwa hatua hii ya kujitosa kushiriki kwani ni hatua kubwa kwa sababu hata mimi nilianzia katika ngazi ya awali kama hii lakini tangu nilipoingia katika shindano hilo nilijiona ni mshindi hali iliyonijengea kujiamini hata nilipokwenda katika shindano la Kanda na hatimaye taifa hivyo nawatakia kila la kheri.

Shindano hilo linaloandaliwa na Kampuni ya Linda Media Solution litapambwa na bendi ya Mashujaa huku kiingilio kikiwa ni sh. 10,000 kwa VIP na siti za kawaida sh. 6,000.
Shindano hilo limedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania kwa kupitia kinywaji chake cha Redds Premium Cold, Shear Illusions, Fredito Entertainment, CXC Africa, Multichoice DSTV, Times FM, Michuzi Media Group (MMG), Santorine Holiday Resort ,PR.Promotion, Aco Catering Servises , Amazon Night Club na Panandipanandi Pub .Picha na Michuzi

No comments

Powered by Blogger.