Vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vimeendelea kutokea nchini licha ya kupigwa vita kwa kampeni mbalimbali
Mpwapwa. Katika miaka ya hivi karibuni kumeibuka habari kuhusu ukatili unaofanywa dhidi ya watoto. Hii siyo tena jambo la ajabu.
Baadhi ya ukatili huo ni pamoja na kubakwa na ule wa kukatwa viungo vya mwili kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi (albino).
Licha ya kupigiwa kelele, hata kampeni mbalimbali
za kupinga kufanyika, unyama huo umeendelea kufanyika na tukio la hivi
karibuni limemhusisha mtoto Erisia Tito mwenye miezi miwili anayedaiwa
kunajisiwa wilayani Mpwapwa Mkoa wa Dodoma.
Tukio hilo limekuwa gumzo katika mitaa mbalimbali
wilayani humo, huku baadhi ya wananchi wakidai kuwa linahusiana na imani
za kishirikina.
Unaweza kujiuliza maswali mengi, hata inakuwaje mtoto wa miezi miwili kunajisiwa?
Katika vijiwe vya kahawa wilayani Mpwapwa, hii ni habari kubwa zilizokuwa zikizungumzwa kuhusu kunajisiwa kwa mtoto huyo swali likibaki; Je, yule mtu alimnajisi mtoto ameishia wapi?
Katika vijiwe vya kahawa wilayani Mpwapwa, hii ni habari kubwa zilizokuwa zikizungumzwa kuhusu kunajisiwa kwa mtoto huyo swali likibaki; Je, yule mtu alimnajisi mtoto ameishia wapi?
Naingia chumba cha Mganga Mkuu Wilaya ya Mpwapwa
kupata maelezo ya mtoto huyo tangu alipofikishwa katika hospitali ya
wilaya hiyo, maendeleo yaliyofikiwa na utaratibu wa kiuchunguzi
unavyoendelea.
Kauli ya Mganga Mkuu
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa, Lunemo Sakafu anasema kuwa tangu alipolazwa, mtoto huyo alikuwa akipelekwa kliniki kwa ajili ya kupatiwa chanzo mbalimbali na kupima afya yake, kwamba alikuwa na afya nzuri.
“Hakuzaliwa katika hospitali hii ila alikuwa
akihudhuria kliniki, alizaliwa kwa wakunga wa jadi na mara ya mwisho
kuja hapa hospitali ilikuwa Aprili 15, mwaka huu na alikuwa na afya
nzuri,” alisema
Ashangazwa
Alisema kuwa alishangazwa na hali aliyokuwa nayo mtoto huyo alipofikishwa kwa mara nyingine katika hospitali hiyo kwani alikuwa akitokwa haja zote bila kikomo.
“Tunampatia matibabu ya kina ili kujua tatizo ni
nini. Kwa sasa tuna utaratibu wa kumpeleka katika Hospitali ya Rufaa ya
Dodoma ili akafanyiwe vipimo vya kina kwa kuwa mtoto huyu anatoa haja
zote bila kikomo,” anasema Sakafu.
Sakafu anasema hata wazazi wa mtoto huyo
walipoulizwa juu ya hali aliyonayo mtoto wao, walipishana kauli katika
maelezo yao na kwamba jambo hilo liliwatia shaka.
Kauli za wazazi
Baba wa mtoto huyo, Silvani Msemakweli anasema kuwa tangu mtoto wake alipozaliwa alikuwa na maumivu wakati wa kupata haja kubwa.
Kauli za wazazi
Baba wa mtoto huyo, Silvani Msemakweli anasema kuwa tangu mtoto wake alipozaliwa alikuwa na maumivu wakati wa kupata haja kubwa.
“Tangu alipozaliwa hali hii ilikuwapo hasa wakati
wa kujisaidia haja kubwa mtoto analia, kwani husikia maumivu makali.
Katika ukoo wetu yupo mmoja wa ndugu zetu aliyewahi kuwa na mtoto
aliyekumbwa na hali kama hii ya mtoto wangu,” anasema na kuongeza:
“Yeye alipona baada ya kutumia dawa za kienyeji na alipona kabisa, siyo kweli kuwa mtoto alinajisiwa.”
Msemakweli anaongeza kuwa ni vigumu kuamini kama
mtoto huyo amenajisiwa kutokana na mazingira ya familia hizo mbili,
yaani familia yake na ya mke wake.
“Japo sikuwapo siku hiyo, lakini bado siamini kama
mtoto wangu atakuwa amenajisiwa. Kwa sasa mama yangu ndiyo
anayeshikiliwa na polisi na kufunguliwa kesi,” anasema Msemakweli.
Mama wa mtoto huyo, Rejina Msemakweli anasema kuwa
yeye alijifungua kwa mkunga wa jadi aliyemtaja kwa jina la Hilda
Maderemo na kwamba mtoto alikuwa mzima na hakuwa na tatizo lolote.
Anasema kuwa baada ya kujifungua alianza kumpeleka
mtoto huyo katika Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa kwa ajili ya kupata
chanjo mbalimbali.
“Mwanangu nilimzaa akiwa mzima nilishangaa siku
moja analia sana wakati huo alikuwa amepakatwa na bibi yake,” anasema na
anaongeza:
“Nilimwacha na bibi yake kwa kuwa nilikwenda
shambani ila niliporudi nilimkuta akiwa analia kupita kiasi. Nilimchukua
na kumwogesha, lakini kabla sijamaliza niligundua kuwa ameumia sehemu
zake za siri na alikuwa akitoka kinyesi mfululizo, yaani mbele na
nyuma.”
Regina anaeleza kuwa familia yake ina watoto
wawili ambao wote ni wasichana, mume wake pamoja na mdogo wake wa kike,
kwamba pia wanaishi kwa ukaribu mkubwa na familia ya mume wake.
“Katika maisha yetu nimekuwa nikiishi na wakwe
zangu bila maelewano mazuri, familia imekuwa ni yenye kugombana kila
wakati, hata kama kitu ni kidogo. Lakini yataibuka mambo makubwa kiasi
kwamba utadhani ni watu wasio familia moja inaniuma sana,” alisikitisha.
“Naongea kwa kuvumilia tu, lakini moyoni ninaumia
kwa kiasi kikubwa kuona mwanangu amekuwa katika hali kama hii sielewi.
Tukijaribu kumwuliza mama mkwe wangu hasemi ukweli kuwa mtoto
amekuwaje,” anasimulia Regina huku akilia machozi.
Kauli ya mkunga
Mkunga Hilda Mademo anakiri kuwa alimzalisha Regina na kwamba mtoto huyo alikuwa mzima bila kuwa na kasoro yoyote.
Polisi yatoa tamko
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Polisi David Misime anakiri kupokea taarifa za kunajisiwa kwa mtoto wa miezi miwili katika Kijiji cha Ising’u wilayani Mpwapwa.
Viongozi wa Serikali wakemea
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mkoa wa Dodoma, Ryoba Kangoye amekemea vikali tukio hilo na kuliita ni la ugaidi kwa kuwa mtu huyo hakuwa na nia ya kubaka bali ni kuua.
Viongozi wa dini
Kwa niaba ya madhebu ya dini, Padiri Masasi Deo kutoka Kanisa la Katoliki Mpwapwa, amekemea vikali tabia hiyo akisema:
Haki za binadamu
Mkurugenzi wa Haki za Binadamu (AFNET)Mkoa wa Dodoma, Sara Mwanga amesema kuwa kitendo hiko ni unyama na kwamba jamii bado haina elimu ya kujitambua kuhusu ukatili unaofanywa hasa katika kushughulikia kesi za aina hiyo.
MWANANCHI
Anasema kuwa aligundua kwamba sehemu za siri za mtoto wake
zimevimba na kuonyesha kukwaruzika huku akitokwa na kinyesi bila kikomo.
Kauli ya mkunga
Mkunga Hilda Mademo anakiri kuwa alimzalisha Regina na kwamba mtoto huyo alikuwa mzima bila kuwa na kasoro yoyote.
“Mimi ndiye niliyemzalisha mama huyo na mtoto
alizaliwa akiwa mzima kabisa. Suala la kupatikana kwa tatizo hilo,
ukweli wanao wazazi wenyewe. Huduma zangu nilizitoa hata hospitali ya
wilaya inalifahamu, walinitembelea hadi hapa kuona mazingira
ninayofanyia kazi na kunisaidia baadhi ya vifaa kwa mfano haya
mabakuli,” anasema Hilda.
Polisi yatoa tamko
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Polisi David Misime anakiri kupokea taarifa za kunajisiwa kwa mtoto wa miezi miwili katika Kijiji cha Ising’u wilayani Mpwapwa.
“Sisi tulipokea taarifa hiyo na kuanza kuifanyia
kazi za awali, hadi sasa bibi wa mtoto huyo yuko mikononi mwa polisi.
Tunasubiri jibu la kitaalamu kutoka kwa daktari kwa kuwa wakati mtoto
amepelekwa katika hospitali,”alisema Misime na kuongeza:
“Katika Kituo cha Polisi hapakuwa na ushahidi wa kujitosheleza kwa kuwa mtoto huyo tayari alikwishasafishwa siku tatu zilizopita.”
“Katika Kituo cha Polisi hapakuwa na ushahidi wa kujitosheleza kwa kuwa mtoto huyo tayari alikwishasafishwa siku tatu zilizopita.”
Viongozi wa Serikali wakemea
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mkoa wa Dodoma, Ryoba Kangoye amekemea vikali tukio hilo na kuliita ni la ugaidi kwa kuwa mtu huyo hakuwa na nia ya kubaka bali ni kuua.
“Hii hali siyo ya kawaida ni mstuko mkubwa kusikia
hili kama hiyo kujitokeza katika mazingira hayo. Hivi, Mtanzania wa leo
kufikia kufanya jambo kama hilo ni ajabu kubwa, hata hiyo familia kukaa
kimya ni kunyima haki vyombo vya sheria kufanya kazi zake na kupoteza
ushahidi uliokamika,“ anasema Kangoye.
Mtendaji wa kijiji hicho, Emmanuel Mamba anasema
kuwa waliposikia tukio hilo walijikuta ni kama wamemwagiwa maji au
tindikali wakilifananisha na mauaji.
“Tulioposikia tuliishiwa na nguvu kwa kuwa hata
kama matendo kama hayo hufanyika, basi isingekuwa kwa mtoto mdogo kama
huyo, asiye na uwezo wowote ule. Tulijiuliza maswali mengi hata kuhisi
huenda walitaka kumfanyia ukeketaji,” anasema Mamba
Viongozi wa dini
Kwa niaba ya madhebu ya dini, Padiri Masasi Deo kutoka Kanisa la Katoliki Mpwapwa, amekemea vikali tabia hiyo akisema:
“Nionavyo sasa umefika wakati wa watu wenye
dhamana na jamii kukaa pamoja na kufanya ibada na kujua mbinu mpya ya
kufundisha maadili kutokana na hali ya maadili ilivyobadilika nchini.”
Haki za binadamu
Mkurugenzi wa Haki za Binadamu (AFNET)Mkoa wa Dodoma, Sara Mwanga amesema kuwa kitendo hiko ni unyama na kwamba jamii bado haina elimu ya kujitambua kuhusu ukatili unaofanywa hasa katika kushughulikia kesi za aina hiyo.
“Watoto wengi wamekuwa wakiumizwa, lakini mwishowe hakuna
linalofanyika katika kumtetea mtoto huyo kutokana na wahalifu huachiwa
huru kwa kile kinachodaiwa ushahidi haujakamilika. Kwa kweli kuna utata
mkubwa katika suala hilo,” alisisitiza.
Aliitaka Serikali kupitia vyombo vya dola kuwa
makini katika kuangalia namna ya kupatikana kwa ushahidi ili kutenda
haki kwa watoto wanapoumizwa, badala ya watuhumiwa kuachiwa huru kwa
madai kuwa ushahidi haujakamilika.
No comments:
Post a Comment