*Watuhumiwa kushiriki biashara ya magendo
*Wamo wa vyeo mbalimbali, Kova atoa onyo kali

JESHI
la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limekumbwa na kashfa nzito,
baada ya askari wake 16 kutiwa mbaroni kwa tuhuma za kuwasaidia
wafanyabiashara wakubwa kupitisha biashara ya magendo bila kulipa kodi.
Mtandao huo umekuwa ukivusha mali kupitia bandari bubu zisizo rasmi
maeneo ya Kawe hadi Bagamoyo na kupewa rushwa ili kuwaachia
wafanyabishara hao.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema askari hao wapo chini ya ulinzi na wanaendelea kuhojiwa. Alisema pamoja na askari hao kuhojiwa, mpaka sasa majina ya wafanyabiashara yamefadhiwa kwa sababu bado wapo wengi wanaoendelea kutafutwa.

Alisema mbali na hatua hiyo ambayo imo katika mfumo wa operesheni ya
misako ya kukamata wahalifu, pia wamelenga wafanyabiashara na
wafanyakazi wa taasisi nyingine ambazo zitabainika kuhusika na mtandao
huo.
"Uchunguzi zaidi unafanyika na yeyote atakayebainika amefanya kosa lolote la jinai, atachukuliwa hatua,tunaangalia kwa makini wale wote ambao watabainika hawana hatia tutawaachia,
"Jeshi la Polisi, lipo katika mfumo wa Tehama (teknolojia, habari na mawasiliano), kwa hiyo tutaweza kuwakamata wahalifu wa aina mbalimbali wakiwamo askari wanaojihusisha na vitendo hivyo kinyume na sheria za jeshi la polisi,"alisema Kova.
Kamanda Kova aliwashukuru wananchi kwa jitihada zao ambao waliamua kushirikiana na polisi kubaini uovu unaofanywa na jeshi hilo.
Alisema kazi ya kuendelea kufisha jeshi hilo, itakuwa endelevu na fundisho kwa askari wote wanaokiuka viapo vyao.
Wakati huohuo, jeshi la polisi limekamata bunduki ya Sub Machine Gun (SMG) yenye namba za usajili 235882 na risasi 25 katika eneo la Kimara wilayani Kinondoni na mtutu wa bunduki aina ya Shortgun, ukiwa umefutwa namba za usajili.
Mbali ya risasi hizo, pia polisi walikamata magari kadhaa ambayo yanahofiwa kutumiwa kwenye vitendo vya uhalifu kwa nyakati tofauti.
Miongoni mwa magari hayo, ni aina ya Noah lililokamatwa eneo la Tegeta na Carina ambayo yalikutwa kwa mtuhumiwa Jumanne Athuman (28) mkazi wa Manzese.
Wakati huo huo, polisi inawashikilia watu watatu, kwa kosa la kukutwa na spea mbalimbali za magari katika eneo la Tabata Dambo.

MTANZANIA
No comments:
Post a Comment