Kada wa Chama cha mapinduzi [CCM] Yared Jamal akifafanua jambo wakati alipokuwa akiwatuliza wakulima ambayo mashamba yao yanapimwa na CDA katika kijiji cha nzuguni Dodoma Bila wakulima hao kuwa na taarifa yoyote. (PICHA NA JOHN BANDA)
Mkuu wa Mambo ya kimila wa kabila la kigogo Lazaro Chihoma akimwagilia maji juu ya mnara wa kumbukumbu wananoujenga pembezoni mwa kisima cha maajabu Kilichopo katika mlima wa Bwibwi kijiji cha iyumbu Dodoma.(PICHA NA JOHN BANDA)
Polisi wakiingia kurinda usalama katika eneo linalopimwa na CDA lililopo kijiji cha nzuguni manispaa ya Dodoma bila ya wakulima zaidi ya 100 waliokuwa wakilitumia eneo hilo kuwa wa Taarifa yoyote.(PICHA NA JOHN BANDA)
Wafanyakazi wa Mamraka ya Ustawishaji makao makuu CDA wakipima eneo la wakulima lililopo kijiji cha nzuguni manispaa ya Dodoma huku kukiwa na mzozo kati yao.
Na John Banda, Dodoma
VIONGOZI wa Serikali ya Kata na kijiji cha Nzunguni wameshindwa kujibu madai ya wakulima ambao mashamba yao yanayoendelea kupimwa na mamlaka ya ustawishaji wa makao makuu (CDA) chini ya ulizi mkali wa polisi.
Hali hiyo imejitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa wakulima wa kijiji hicho ulioitishwa na CCM Wilaya ya Dodoma mjini baada ya chama hicho kungundua viongozi hao wameshindwa kuitisha vikao wa kutoa ufafanuzi wa uhalali wa CDA kupima katika maeneo ya mashamba yao.
GAZETI hili ambalo iliikuwepo kwenye mkutano huo viongozi hao walijikuta wakiwa mabubu na kushinndwa kujibu maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wakulima hao,hali ambayo ilionekana moja kwa moja wanatuhumiwa kushiriki katika uvamizi huo, ambapo mwakilishi wa CCM Yared Jamal aliwaokoa kwa kutuliza jaziba za wakulima hao.
Wakulima walisema kutokana na hali hiyo hivi sasa hawana imani na viongozi hao wa serikali ya kata na kijiji, kutokana na kujimilikisha maeneo waliyokuwa wakiyatumia kwa kilimo kwa kivuli cha Mamlaka ya Ustawishaji wa Makao Makuu (CDA)
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika madai yao wakulima hao walisema kuwa wanatuhumu viongozi kwa kuuza maeneo ya mashamba yao baada ya kuwaona hawana ushirikiano ambao ungeweza kuwafafanulia juu ya upimaji unaoendelea kwa hivi sasa katika maeneo hayo.
Mmoja wa wakulima Joryjetanas Pasua alisema viongozi hao wanaotuhumiwa ndiyo wamekuwa chanzo cha kuwaleta CDA kuja kupima na ndiyo maana wakulima hatuna imani nao.
Rebart Magelanga alisema viongozi hao wameshindwa kutekeleza utendaji wao kwa kupitia katiba ya nchi na ndiyo inavyoonekana kwa uapande wao kuhusika moja kwa moja kutuhumiwa na kashifa hiyo ambayo isingefikia hapo.
‘’Ninyi viongozi hamjitambui kwamba nani afanye nini na mwingine kipi ndiyo maana mnafanya kinyume na mnavyotakiwa, kama vile maagizo ya utekelezaji yatokayo kwa viongozi wakuu hatuambiwi kiasi cha leo kutuambia hati ya kijiji kufutwa wakati sisi, katika haya kwanini msiwajibishane kwa manufaa ya serekali?’’, alisema Magelanga
Aidha aliongeza kuwa viongozi hao kutoitisha mikutano ya hadhara ambayo wangeweza kutoa elimu juu ya CDA ambayo imedharau hata hati iliyotolewa na marehemu Mwalimu Nyerere mwaka 1972 badala yake ni kuwaburuza wananchi.
Magelanga alisema kutokana na hali hiyo sisi wakulima tunaamini na kuwatuhumu kuwa kwa asilimia mia mmoja uongozi wa serikali wameuza eneo hilo.
Kwa upande wake Yared Jamal ambaye alimwakilisha Katibu wa CCM Wilaya ya Dodoma Saad Usilawe aliwataka viongozi wa kata na kijiji kushirikiana na wakulima wao ili kuzuia vurugu ambazo zinazoweza kutokea ikiwa hawatawa shirikisha.
Jamal aliwaambia viongozi hao kuhakikisha wanashirikiana na wakulima hao zaidi ya 100 kuweka sawa jambo hilo la Upimwaji katika eneo husika, huku akiwatahadharisha kuwa CCM hakitaki kuona wananchi wakinyanyasika wakati viongozi wao wapo.
‘’Sikilizeni Viongozi na wakulima kila mtu anayesikia kuhusu CDA anajisikia vibaya kutokana na mfumo wao wakirusiwa kupima au kuvunja nyumba 7 wao wanavunja 20 hivyo kuweni makini , pia iundwe kamati ya watu 5 waongezwe kwenye idadi ya wakulima waliopitiwa na upimaji huo iletwe CCM wilaya ili tatizo hilo litafutiwe ufumbuzi’’, alisema.
Aliongeza kuwa upimaji huo ulioanza kuanzia Jumatatu wiki hii itabidi usimame wakati ufumbuzi kuhusu wakulima hao unashughulikiwa.
Hali hiyo imekuja baada ya CDA kutinga katika eneo la nzuguni mwanzoni mwa wiki na kuanza upimaji huku wakilindwa na jeshi la polisi, huku wakulima wenye mashamba wakihaha kuwapata viongozi wao bila kupata mafanikio baada ya kila aliyetafutwa Kuanzia Diwani wa kata hiyo Chiwanga Magongo, Afsa mtendaji wakata Vicent Leo, wa kijiji Jackson Leuna, mwenyekiti wa mtaa Michael Samwel na hata Katibu Jane Masese wote kuwa na Udhuru.






.jpg)

No comments:
Post a Comment