HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » HESLB:ZINGATIENI MUDA WA KUOMBA MIKOPO

Mkurugenzi wa Mawasiliamo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Cosmas Mwaisobwa
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa msisitizo kwa wanafunzi waliohitimu kidato cha sita mwaka huu na kujiunga va vyuo vya elimu ya juu kuanza mara moja na kuzingatia ratiba kuomba mikopo hiyo.
Mkurugenzi wa Mawasiliamo wa Bodi hiyo, Cosmas Mwaisobwa aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kuwa, wanafunzi hao wanatakiwa kuanza kujaza fomu za maombi na kusisitiza kuwa siku ya mwisho ya kupokea maombi hayo ni Juni 30 mwaka huu.
“Bodi inasisitiza kuanza mchakato wa kuomba mikopo kwa waliomaliza kidato cha sita na kuzingatia muda uliotolewa kujaza fomu za maombi na kuziwasilisha kwenye ofisi za bodi,” alisema.
Akizungumzia kuhusu wanafunzi wanaoendelea na masomo, Mwaisobwa alisema tayari waombaji 62,758 wamekamilisha taratibu za maombi ya mikopo na kujaza fomu stahiki tangu utaratibu huo ulipozinduliwa rasmi Mei Mosi mwaka huu.
“Hadi sasa mchakato kwa waombaji wa mikopo kwa wa mara ya kwanza na wanafunzi wanaoendelea na masomo unaendelea vizuri ambapo wengi wameweza kujaza fomu za maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao,” alisema.
Aidha, Bodi ya mikopo imewataka waombaji kuzingatia maelezo yaliyotolewa wakati wa ujazaji wa fomu hizo na kuhakikisha wanakamilisha mchakato huo haraka ili kutoa nafasi kwa bodi kuchambua maombi hayo na kupanga madaraja ya mikopo kwa waombaji.
Katika mwaka wa masomo wa 2012/13, Bodi hiyo iliwapatia mikopo waombaji 94,703, ambao wako katika vyuo na taasisi mbalimbali za elimu ya juu hapa nchini.
 
CHANZO: NIPASHE

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: