Picha juu na chini ni Washiriki 11 wa Redd's Miss Kigamboni wakifungua shindano hilo kwa show ya aina yake.
Wanenguaji wa Bendi ya
FM ACADEMIA maarufu kama Wazee wa Ngwasuma wakitoa burudani wakati wa
shindano la kumsaka Redd's Miss Kigamboni 2013 lililofanyika usiku wa
kuamkia leo kwenye ukumbi wa Navy Beach Kigamboni jijini Dar.
Pichani juu na chini washiriki wa Redd's Miss Kigamboni wakipita jukwaani mavazi ya ubunifu.
Washiriki wa Redd's Miss Kigamboni 2013 ndani ya Beach Wear.
Mmoja wa majaji ambaye
pia ni Mkurugenzi wa CXC Tours and Safari Bw. Charles Hamka akitangaza
majina ya warembo waliofanikiwa kutinga tano bora.
Washiriki wa Redd's Miss Kigamboni waliofanikiwa kutinga tano bora.
Aliyewahi kushika taji
la Miss Tanzania 1999 Hoyce Temu ambaye pia ni Somo wa washiriki wa
Redd's Miss Kigamboni 2013 akiwauliza maswali washiriki waliofanikiwa
kutinga tano bora kwenye shindano hilo.
Washiriki wa Redd's Miss Kigamboni 2013 wakijibu maswali.
Mgeni
rasmi katika shindano la Redd's Miss Kigamboni 2013 Mbunge wa jimbo la
Kigamboni Mh. Dr. Faustine Ndugulile (CCM) akiwa ameambatana na Meneja
Masoko Taifa wa shirika la ndege la Precision Air Bw. Ibrahim Bukenya
wakiwasili ukumbini.
Meza
ya Majaji ikiongozwa na Chief Judge Mwandaaji wa Miss Temeke Bw. Benny
Kisaka (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa CXC Tours and Safari Bw. Charles
Hamka ( wa pili kulia), Mratibu wa Miss Ilala Juma Mabakila (Kushoto)
na Mkuu wa Radio France nchini Bw. Victor Willy (kulia).
Mwandaaji wa mashindo ya Redd's Miss Kigamboni 2013 Angella Msangi akiteta jambo na Chief Judge wa mashindano hayo.
Wadau wa tasnia ya urembo wakishangilia baadhi ya washiriki waliokuwa wakijibu maswali yao bila kutetereka.
Miss Kigamboni 2012 Edda Slyvester anayemaliza muda wake akisubiri kukabidhi taji kwa Redd's Miss KIgamboni 2013.
Miss Kigamboni 2012
Edda Slyvester aliyemaliza muda wake akimvisha taji mshindi wa shindano
la Redd's Miss Kigamboni 2013 Magdalena Olotu (aliyeketi) wakati wa
shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Navy
Beach Kigamboni jijini Dar.
Mshindi wa Redd's Miss
Kigamboni 2013 Magdalena Olotu (katikati) akila pozi katika picha ya
ukumbusho na mshindi wa pili Latifa Mohamed( wa pili kulia) na Mshindi
wa tatu Irene Rajab ( wa pili kushoto) pamoja na mshindi wa nne na wa
tano.
Mgeni rasmi katika
shindano la Redd's Miss Kigamboni 2013 Mbunge wa jimbo la Kigamboni Mh.
Dr. Faustine Ndugulile (CCM) akitoa nasaha zake kwa mshindi wa taji la
Redd's Miss Kigamboni 2013 Magdalena Olotu mara baada ya kuibuka kidedea
wa taji hilo ambapo amemtakia Baraka zote kuiwakilisha vyema Kigamboni.
Mgeni rasmi katika
shindano la Redd's Miss Kigamboni 2013 Mbunge wa jimbo la Kigamboni Mh.
Dr. Faustine Ndugulile (CCM) akimkabidhi zawadi ya fedha taslimu
shilingi 500,000/mshindi wa taji la Redd's Miss Kigamboni 2013 Magdalena
Olotu iliyotoka mfukoni kwa Mbunge huyo.
Meneja Masoko Taifa wa shirika la ndege la Precision Air Bw. Ibrahim Bukenya akikabidhi zawadi ya fedha taslimu shilingi 250,000/ kwa mshindi wa tatu wa Redd's Miss Kigamboni 2013 Irene Rajab.
Mwenyekiti wa Kamati ya
Miss Tanzania, Bw. Prashant Patel katika pozi na mshindi wa pili wa
shindano la Redd's Miss Kigamboni 2013 Latifa Mohamed mara baada ya
kumkabidhi zawadi ya fedha taslim shilingi 300,000/.
Redd's Miss Kigamboni
2013 Magdalena Olotu katika pozi na kitita chake cha fedha taslim
shilingi 500,000/ zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Mh. Dr.
Faustine Ndugulile
Raia wa kigeni kutoka
China aliyehudhuria shindano la Redd's Miss Kigamboni 2013 akichukua
picha ya ukumbusho ya mshindi wa taji hilo.
Mwandaaji wa shindano la Redd's Miss Kigamboni 2013 Angella Msangi (kulia) na Mratibu wa shindano hilo, Somoe Ng’itu pamoja na Meneja
Masoko Taifa wa shirika la ndege la Precision Air Bw. Ibrahim Bukenya
(kushoto) wakati wa zoezi la kukabidhi zawadi kwa washindi.
Raia wa Kigeni kutoka china ndani Redd's Miss Kigamboni 2013.
Picha juu na chini ni
baadhi ya Wadau wa tasnia ya masuala ya Urembo kutoka sehemu mbalimbali
za jiji la Dar waliohudhuria shindano la Redd's Miss Kigamboni 2013.
Nyomi ya Ukweli na Clouds Tv walikuwepo kuhakikisha shindao hilo linaruka Live.
Aliyewahi kushika taji
la Miss Tanzania 1999 Hoyce Temu ambaye pia ni Somo wa washiriki wa
Redd's Miss Kigamboni 2013 akifurahi jambo na baadhi ya wageni
waalikwa.(Picha zote na Zainul Mzige wa Dewjiblog).
No comments:
Post a Comment