MAMA AKAA SIKU TATU JUU PAA LA NYUMBA YAO KUPINGA ISICHUKULIWE NA BENKI YA TANZANIA INVESTMENT BANK (TIB)


 Huyu mama alikaa juu ya paa kwa siku tatu tangu jumamosi kupinga nyumba yao kuchukuliwa na bank.Anasema mumewe alimdhamini mtu alipochukua mkopo bank miaka mingi iliyopita na kushindwa kulipa mkopo huo.(Picha ni kwa Hisani ya Clouds Fm)
 Huu ndio mwonekano mzuri wa mama wakati yuko juu ya paa la nyumba ambayo imechukuliwa na Benki ya Tanzania Investment bank(TIB)
 Gea alimfata huko huko juu kumsikiliza na tumemsikia leo kwenye heka heka.Kesho pia itaendelea.
Nyumba ipo mbezi Tangi bovu na inaeneo kubwa sana mama anasema hata akiuza si chini ya millioni 500 na iweje atolewe kwa milioni 240? Wakati mdaiwa nyumba zake mbili zimeshachukuliwa na mabasi mawili yale makubwa ya safari za mikoani.Hiyo milioni 240 haijatimia tu? na kama bado kiasi gani kimebaki?

Kwa mujibu wa maelezo yake kesi yao bado ipo mahakamani kwani tayari yule mdaiwa kuna mali zake zilizotaifishwa.
Mdaiwa alikopa milioni 240 wameuza nyumba zake mbili (2) na mabasi mawili. Wenyewe wanachodai katika hilo deni imebaki shilingi ngapi za kitanzania na wao watoe maana wanauwezo wa kulilipa deni lililobaki ilinyuba yao isichukuliwe na benki? Na kama nyumba ikiuzwa watoe deni la bank na hela inayobaki wabaki nayo wao.

Maana wakati haya yakiendelea hiyo jana inasemekana hii nyumba imeshauzwa.Inauzwaje na shauri lipo mahakamani?Na jana mume wa huyu mama alikuwa mahakamani maana ilikuwa siku ya kesi kuendelea kusikilizwa.
Na mumewe alirudi na oda maalum kutoka mahakamani kuwa nyumba hiyo isiguswe na vitu vyao virudishwe.
Inavyoonekana hapa watu wameishakula pesa ili nyumba hii iuzwe wakati ni kinyume cha sheria na istoshe kesi iko mahakamani kwa viongozi wetu jaribuni kulifuatilia suala hili ili mwenye kupata haki yake apate na sio kutumia mabavu wakati nchi hii ni yetu wote

No comments

Powered by Blogger.