MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Lionel Messi na baba yake, Jorge watapanda kizimbani katika Mahakama ya Hispania Septemba katika sehemu ya kujibu tuhuma zao za kukwepa kodi.
Wawili hao wametakiwa kuhudhuria Mahakamani Gava, Catalonia, Jumanne ya September 17 kujibu maswali ya kukwepa kodi Hispania kiasi chaEuro Milioni 4 (Pauni Milioni3.4) kati ya mwaka 2007 na 2009.
Taarifa kutoka kwa Waziri wa Sheria imesema: "Korti namba 3 ya Gava imekubali imekubali kufungua mjadala uliowasilishwa na mwendesha mashitaka dhidi ya Lionel Andres Messi na Jorge Horacio Messi kwa mashitaka matatu dhidi ya Wizara ya Fedha, kuhusiana na ukwepaji kodi kwa miaka ya 2007, 2008 na 2009 na akikutwa na hatia atafungwa jela miaka sita.
Nyota huyo wa Argentina, Messi, mwenye umri wa miaka 25, wiki iliyopita aliandika katika ukurasa wake wa Facebook akikanusha kuhusu yeye au baba yake kuhusika uovu wowote.
Taarifa ya Mwanasoka huyo bora wa Dunia wa FIFA imesema: "Tunafahamu kupitia vyombo vya habari kuhusu madai yaliyofunguliwa na Mamlaka ya Mapato ya Hispania
No comments:
Post a Comment