HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » MOURINHO ATIMKA REAL MADRID KWA KISHINDO BILA JEMBE LAKE, RONALDO

Last act: Jose Mourinho took charge of his final match at Real Madrid on Saturday 
Jose Mourinho akiwa kocha wa Real Madrid kwa mara ya mwisho usiku huu katika dimba lake santiago Benabeu
Snappers: Mourinho was surrounded by photographers on the touchline on Saturday at the Bernabeu 
Waandishi wa habari wakimpiga picha za mwisho kocha Jose Mourinho akiwa kocha wa real Madrid kwa mara ya mwisho
Cheers and jeers: Mourinho was greeted with a mixed reaction during Real Madrid's match against Osasuna
Mourinho amesalimiwa kwa mgawanyiko uwanjani, kuna waliomshangilia na walioonesha kutofurahishwa na tabia za kocha huyo klabuni hapo, duniani huwezi kupendwa na watu wote.
Appreciation: A Real Madrid supporter waves a Mourinho flag during his farewell match
Mashabiki wa  Real Madrid wakipeperusha bendera ya Mourinho kuonesha heshima kwake na kukubali kazi yake klabuni hapo.
 Gracias: Real fans hold up messages saying 'thank you' to their departing Portuguese managerMashabiki wa Real Madrid wakishika makaratasi yenye ujumbe wa shukurani kwa kocha Jose Mourinho anayeondoka klabuni hapo
Farewell: Mourinho waves goodbye to the fans after the match in Madrid
Mourinho akiwaaga mashabiki wa Real Madrid baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa
 Real Madrid's Portuguese coach Jose MourinhoReal Madrid's coach Jose Mourinho
Mourinho akiwapungia mikono mashabiki na wapenzi wa Real Madrid alipomaliza mechi ya mwisho
Stare: Cristiano Ronaldo was left out of the final match of the season by Mourinho with a back injury 
Ronaldo aliachwa katika kikosi cha leo kutokana na majeruhi Ovation: Ronaldo greeted the crowd before kick off in the La Liga match at the Bernabeu
Ronaldo  aliingia uwanjani na kuwasalimia mashabiki wa klabu yake
Lead: Gonzalo Higuain gave Real Madrid the lead in the first half
Bao la kuongoza: Gonzalo Higuain akipongezwa baada ya kutia gozi kimiani
 Familiar face: Michael Essien, who worked with Mourinho at Chelsea, doubled Madrid's lead before half-timeWanafamilia wamekutana: Michael Essien aliyefanya kazi na Mourinho akiwa Chelsea, aliifungia Real Madrid bao la pili katika mchezo wa leo usiku.

Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Mourinho “byee byee’” Real Madrid!, amemaliza kazi, sasa njia nyeupe kurudi zake kuelekea darajani nchini England kurithi mikoba ya kocha wa muda wa chelsea Rafa Benitez.
Ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Osasuna ambao klabu ya Real Madrid imepata katika mechi ya kufunga pazia la Ligi kuu nchini Hispania usiku huu, umemfanya kocha wa klabu hiyo Mreno Jose Mourinho aage kwa furaha baada ya kuruhusiwa kuondoka klabuni hapo na kutajwa kurejea katika klabu yake ya zamani ya Chelsea ya nchini Uingereza.
Mabao ya Real Madrid yametiwa kimiani na wachezaji Gonzalo Higuain dakika ya 35 kipindi cha kwanza, Mickael Esien katika dakika ya 38, Karim Benzema dakika ya 69 na Jose Maria Callejon.
Kipute hicho cha mwisho kwa Mourinho akiwa kocha wa Real kimepigwa katika dimba la Nyumbani Santiago Bernabeu na kushuhudiwa na mashabiki lukuki wa miamba hiyo ya soka barani ulaya.
Katika mchezo wa leo nyota kadhaa wa Real Madrid hawajatia madaluga yao uwanjani akiwemo mchezo nyota Mreno Cristiano Dos Santos Aveiro Ronaldo anayesumbuliwa na majeruhi.
Nyota huyo anawindwa na klabu yake ya zamani ya Manchester United pamoja na wazee wa darajani Chelsea.
Umekuwa historia nzuri kwa Mourinho ambaye ameandika katika mtandao wa klabu hiyo akiaga kwa ushindi mnono dhidi ya Osasuna baada ya kukaa miaka mitatu nchini Hispania akinoa makali ya Real Madrid.
Baada ya kumalizika kwa mechi, Mourinho ambaye amekubali kurejea Chelsea msimu ujao wa ligi kuu nchini England aliwapungia mkono mashabiki wa klabu yake akiwapa mkono wa kwaheri.
Akizungumza na wanahabari Mourinho amekaririwa akisema “Natamani kuwaona mashabiki wa Real Madrid wakiwa na furaha wakati wote. Nawashukuru sana mashabiki wa sapoti yao, naheshimu walivyokuwa wananikosoa. Narudia tena nawatakiwa mashabiki furaha zaidi na afya njema kwao”.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: