HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » NJAA YATOROSHA WANAFUNZI SHULENI


Wanafunzi wakinunua vitafunwa

Ukosefu wa chakula cha mchana katika Shule ya Sekondari Kimochi iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro chanzo cha baadhi ya wanafunzi kukithiri kwa utoro kutokana na njaa wakati wa masomo nyakati za jioni.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Shule hiyo, Karimu Msangi, tatizo hilo linatokana na wazazi kutochangia fedha kwa ajili ya kunua chakula kwa ajili ya mlo huo kusabaisha kushuka kwa kiwango cha elimu shuleni hapo.
Alisema utoro na  matumizi ya dawa za kulevya kwa baadhi ya wanafunzi kumesababisha  matokeo ya mitihani ikiwamo ya kitaifa kuwa mabaya na kushuka kwa kiwango cha elimu shuleni hapo. 

“Watoto hawapati chakula cha mchana na wakati mwingine hata majumbani walipotoka hawakupata kifungua kinywa ni vigumu kumfundisha mwanafunzi wa aina hii na pia ni vigumu kupata matokeo mazuri kitaaluma... wazazi wamekuwa ni wagumu sana katika kuchangia, ”alisema Msangi
Msangi aliongeza kuwa katika uchunguzi wake amebaini kuwa wanafunzi wengi wanaporuhusiwa kurudi nyumbani,  wanaishia kuzurura mitaani na wengine kujiingiza katika makundi ya matumizi ya madawa ya kulevya.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kimochi,  Samweli Meta aliliambia NIPASHE kuwa  uongozi wa kijiji umejipanga kuwafuatilia wazazi hao na kurudisha utaratibu wa wanafunzi kupata mlo wa mchana shule zitakapofunguliwa ili waendelee na masomo.
Diwani wa Kata ya Kimochi, Ananyisa Macha  aliwataka wazazi  ambao hawajalipa michango mbalimbali shuleni hapo kuwasilisha kabla ya Agosti mwaka huu, vinginevyo watachukuliwa hatua za kisheria.
CHANZO: NIPASHE

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: