Baadhi ya websites zimeandika kuwa Brother Dully Sykes hakwenda kuupokea
wala kuuaga mwili wa marehemu Albert Mangwea “Ngwair” , na badala yake
alikuwa akila bata na mpenzi wake. Ukweli ni kwamba siku moja baada ya
kifo cha marehem Ngwea, Dully alikwenda Mwanza, na alikaa huko kwa siku
mbili. Alipokua anarudi kutoka Mwanza, kwa kuwa alikuwa akiendesha gari
mwenyewe, Dully aliamua kubaki Morogoro tangu Jumatatu kuusubiri mwili
wa Ngwea. Hivyo Dully hakuwa akifanya starehe, bali alikua yupo na
Afande Sele na wananchi kibao maeneo ya Nane nane, wakisubiri
kuusindikiza mwili wa marehemu kutoka maeneo hayo
-
No comments:
Post a Comment