Askari wa Vikosi vya Ulinzi na
Usalama Kisiwani Pemba, wakiwa katika zoezi la kutoa miili ya marehemu
waliopoteza maisha katika ajali ya kuangukiwa na ukuta wa tanki la maji
eneo la Machomanne Chake Chake Pemba leo.
Askari wa JWTZ, kwa kushirikiana na Askari wa vikosi vya SMZ,
wakiingiza miili ya marehemu iliyoangukiwa na ukuta wa tangi la Maji
Machomanne, katika gari ya kubebea wagonja Ambalesi kwa kuipeleka katika
hospitali ya Chake Chake
ASKARI wa vikosi vya Ulinzi na Usalama kisiwani Pemba, wakiutoa mwili
wa Marehemu juu ya Mnara wa tangi la Maji Machomanne, ulioangukiwa na
ukuta wa tangi hoo
Wananchi wakiuangalia mnara wa tangi la maji ulioanguka na kupoteza maisha ya wananchi watatu leo asubuhi.
Mwili wa mmoja wa marehemu ukishushwa kutoka katika mnara huo.
Daktari bingwa kutoka Cuba
anayefanya kazi zake Kisiwani Pemba, (jina halikufahamika) akimtibu
mmoja kati ya majeruhi waliolazwa katika hospitali ya Chake Chake baada
ya ajali hiyo.
Mkuu wa mkao wa kusini Pemba, Juma Kassim Tindwa, akimfahamisha jambo waziri wa Nnchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed, walipofika katika Hospitali ya Chake Chake, kuaangalia majeruhi waliolazwa katika hospitali hiyo.
Mkuu wa mkao wa kusini Pemba, Juma Kassim Tindwa, akimfahamisha jambo waziri wa Nnchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed, walipofika katika Hospitali ya Chake Chake, kuaangalia majeruhi waliolazwa katika hospitali hiyo.
Wananchi wakiwa katika hospitali ya Chake Chake kuwaona ndugu zao na kutambua miili.
JUMLA ya watu watatu wamefariki dunia papo hapo na watatu kujeruhiwa
baada ya kuangukiwa na ukuta wa mnara wa tanki la maji uliopo
Machomanne Chake Chake Pemba, leo saa tatu asubuhi.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kusini Pemba, Suleiman Hassan Suleiman, amesema kuwa, merehemu hao
walifikwa na mauti wakiwa katika kazi ya kuteremsha ukuta wa mnara wa
tanki la maji ambao walikuwa wameshaukata.
Kamanda alisema kuwa idadi ya mafundi waliokuwepo kazini hapo
walikuwa ni 12 ambapo watatu wamepoteza maisha papo hapo na watatu
kujeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya Chake Chake na wengine sita
walikimbia na jeshi la polisi liko katika utaratibu wa kuwatafuta kwa
ajili ya kuelewa hali zao.
Kamanda Suleiman aliwataja marehemu hao kuwa ni Juma Rashid Juma (35)
mkazi wa Chanjaani, Suleiman Mohammed Abdiadi 'maarufu kama Golo' (55)
mkazi wa Kwale na Salum Muhidini Vuai 'Bandudu' (35) mkazi wa Madungu
wote wakazi wa wilaya ya Chake Chake mkoa wa Kusini Pemba.
Na majeruhi katika ajali hiyo ni pamoja na Jackson John (26) mzaliwa
wa Iringa na mkazi wa Msingini, Ali Saleh Ali (35) mkazi wa Michakaeni
na Yohana Richard (25) mkazi wa Machomanne Chake Chake Pemba.
SOURCE: GPL NA ZANZINEWS
No comments:
Post a Comment