Jukwaa liko tayari kwa Show Babkubwa itakayoangushwa na Wasanii mbali mbali waliopo kwenye Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013 ndani ya Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma hivi sasa.ambapo leo hii ni sherehe ya wakazi wa Dodoma Kiburudani.
Dj akiwa tayari tayari kwa kuangusha Bonge moja la Burudani.
Mabaunsa wakiwa tayari washajipanga kwa kazi moja.
Mlangoni mambo yako namna hii,kama huna tiketi inakula kwako.hata hivyo kiingilio ni buku 2 tu (elfu mbili ya kitanzania)
Hii ni Foleni ya Kuingia uwanjani .
Sehemu ya kukatia tiketi nako mambo yapo namna hii,yaani ni full Kikwetu kwetu.
Wako kwenye foleni ya kuingia.
Hata hawa jamaa pia wako hii ni katika sehemu ya kuhakikisha ulinzi umehimarika.
Wazee wa East Afrikan TV wakiwa kamili kamili Uwanjani hapa.
Kamera Man wa EATV mzigoni.
Othman Michuzi( wa kwanza kulia) akikiwa na waendeshaji wa Tamasha hili,Zembwela na Dullah Ambua.
Othman Michuzi( wa kwanza kulia) akikiwa na waendeshaji wa Tamasha hili,Zembwela na Dullah Ambua.
Wazee wa kazi.
"Asie na Tiketi asisogee hapa."
Wakazi wa Dodoma wakiwa wamejitokeza kwa Wingi ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Linex akiwasalimia mashabiki na wapenzi wa Muziki waliofurika kwa wingi ndani ya Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma leo,ambapo usiku wa jana kulikuwa na bonge moja la Show ya Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013.
Linex akikamua kisawasa ndani ya uwanja wa jamhuri mjini Dodoma usiku wa jana.
Msanii aliejinyakulia Tuzo kadhaa za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013,Ommy Dimpoz akienda sambamba na timu yake ya Madansa wakitoa burudani ya kufa mtu ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma usiku wa jana.
Endelea kutizama tukio hili kwa kubofya hapa chini
Msanii Ben Pol akighani moja ya nyimbo zake.
Mashabiki hawakutaka kabisa kupitwa na taswira za show hii.
Ben Pol akiendelea kuwakilisha.
Ni shangwe kwa kwenda mbele ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
Kala akipagawisha mashabiki.
PICHA NI KWA HISANI YA OTHMAN MICHUZI WA MTAA KWA MTAA




















































No comments:
Post a Comment