Mtoto wa kiume nchini China aliyezaliwa na macho ya blue kama ya paka, aliwastaajabisha madaktari baada ya kugundulika kuwa macho hayo yana uwezo wa kuona katika giza totoro bila mwanga wa aina yoyote.
Kwa mujibu wa taarifa iliyosambaa mtandaoni mwaka jana, Nong Youhui aligundulika kuwa na uwezo huo baada ya baba yake kumpeleka hospitali huko Dahua, kusini mwa China kutokana na kuwa na macho yenye mwanga wa blue, lakini madakrati walimwambia hana tatizo lolote.
Vipimo ya madaktari vilionesha kuwa Nong Youhui anauwezo wa kuona na kusoma vizuri kabisa katikati ya giza nene bila msaada wa mwanga wowote kama ambavyo watu wa kawaida wanaona wakati wa mchana.
Kwa mujibu wa World Record Academy (shirika la kimataifa linaloongoza kuzithibitisha rekodi za dunia), Youhui ameweka rekodi ya kuwa bianadamu wa kwanza anayeweza kuona gizani bila mwanga.
No comments:
Post a Comment