.jpg)
Mwangosi aliuwawa katika kijiji hicho Septemba 2, mwaka jana kwa kulipuliwa na kitu kinachodaiwa kuwa bomu baada ya kutokea vurugu kati ya wafuasi wa Chadema na polisi.
Katibu wa Chadema jimbo la Mufindi Kusini, Emmanuel Ngwalanje, akizungumza na NIPASHE jana alisema mnara huo ambao utagharimu kiasi cha Sh. 3,500,000 utaanza kujengwa Agosti 20 na kukamilika Agosti 28, mwaka huu na kuwaomba wadau kusaidia fedha kufanikisha ujenzi huo.
Ngwalanje alisema mmiliki wa eneo alipouwawa Mwangosi amekubali kutoa kibali cha kujengwa mnara huo, hivyo baada ya ujenzi kukamilika Septemba 2, mwaka huu ambayo ni siku aliyouwawa, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Willbrod Slaa, ataweka jiwe la msingi na kuzungumza na wananchi.
Alisema siku hiyo pia kutafanyika harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia mjane wa Mwangosi na watoto wake.
Katibu huyo aliwataka wadau kusaidia kuchangia gharama za ujenzi wa mnara huo ili ujenzi uanze haraka na kukamilika kwa wakati.
Endelea kusoma hanari hii kwa kubofya hapa chini
Kabla ya kuuawa kwa mwanahabari huyo, mabomu yalipigwa eneo hilo ili kuwatawanya wafuasi wa Chadema ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa hawapo tayari kuondoka katika ofisi yao.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment