Eto’o akionesha jezi yake baada kusaini Chelsea jana
Eto’o akisaini mkataba mbele ya katibu na mkurugenzi wa Chelsea David Barnard
Nimefurahi kuwepo hapa: Eto’o amesaini kwa uhamisho wa bure na amesema amefurahi kuwepo darajani.
Endelea kusoma habari hii kwa kubofya hapa chini
Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
KLABU ya Chelsea imethibitisha kumsajili bure mshambuliaji raia wa Cameroon, Samuel Eto’o .
Nyota
huyo mwenye umri wa miaka 32- inafahamika kuwa amesaini mkataba wa
mwaka mmoja kwa dau la pauni milioni 7 , japokuwa atapunguziwa mshahara
wake kwani mpaka sasa ndiye alikuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi
zaidi duniani, dau la pauni milioni 17 kwa mwaka katika klabu ya Anzhi
Makhachkala.
Kocha
wa Chelsea, Jose Mourinho amekata tamaa kumshawishi mshambuliaji wa
Manchester United, Wayne Mark Rooney baada ya ofa zake kutupiliwa mbali
na David Moyes, na sasa amegeukia mpango B ambapo amelinasa jembe hilo
la Kiafrika.
Mourinho
na Eto’o wamekutana tena kwani walishawahi kufanya kazi pamoja katika
klabu ya Inter Milan na kutwaa kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya.
No comments:
Post a Comment