Msaani mwenye kipaji cha Hali ya juu nchini na Mwenye umri mdogo
Elizabeth Michael "LULU"anatarajia kuzindua filamu yake ya Kwanza tokea
alipotoka Gerezani, Filamu hii iitwayo FOOLISH AGE
ikiwa imetengezwa na
Kampuni ya Proin Promotions Limited itazinduliwa leo tarehe 30 August
2013 Katika Ukumbi wa Mlimani city jijini Dar Es Salaam.
Filamu hiyo
inayoelezea Maisha ya kila binadamu katika kila hatua anayopitia katika
ukuaji wake.Ni moja ya filamu nzuri na yenye ubora wa
hali ya juu kutokana na Sauti,Picha hadi maeneo yaliyotumiwa kucheza
filamu.Pamoja na kuwepo lulu humo pia utamuona Msanii Mkongwe
Jengua.Filamu hiyo imetengenezwa na Kampuni ya Proin Promotions
Limited na Itakuwa ikisambazwa Na Proin Promotions Limited.Katika
Uzinduzi huo wa Filamu hiyo ya Lulu Wasanii mbalimbali
akiwemo mwanamuziki Lady Jaydee na Machozi Band anatarajiwa kushusha
bonge moja la burudani ya kufa mtu.
No comments:
Post a Comment