HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » MUME AUAWA KWA KUMNYONGA MKEWE HADI KUFA




Mkazi wa Kijiji cha Kisangwa Kata ya Mcharo wilayani hapa Mkoa wa Mara, Batule Masanja, anadaiwa kumuua mkewe kwa kumnyonga shingo kwa mikono yake kisha naye  kuuawa na wananchi.

Polisi wilayani hapa wamethibitisha kutokea kwa mauaji hayo ya kutisha usiku wa kuamkia juzi katika Kijiji cha Kisangwa Kata ya Mcharo, kwenye sherehe ya ufunguzi wa nyumba ya  ndugu wa wanandoa hao kijijini hapo.  Afisa Mtendaji wa Kata hiyo, Waziri Kingi alimtaja mwanamke aliyeuawa kwa kunyongwa na mumewe kuwa ni Paulina Samson Misinzo.

Kingi alisema Masanja naye aliuawa baada ya kukamatwa na wananchi hao mlimani alikokimbilia kujificha.

Inadaiwa kuwa siku ya tukio hilo Masanja aliyekuwa ametegana na mkewe kwa zaidi ya miezi miwili baada ya kutokea ugomvi wa kifamilia, alimfuta mwenza wake huyo kwenye sherehe hiyo usiku.

Inadaiwa kuwa baada ya kufika nyumbani hapo huku akiwa na watoto wao wawili, alimuita mkewe huyo aliyekuwa akicheza muziki na kumpeleka nyuma ya nyumba ambako inadaiwa alimuua kwa kumnyonga kwa kutumia mikono yake hadi kufa.

Endelea kusoma habri hii kwa kubofya hapa chini

Inaendelea kudaiwa kuwa baadaye alibeba mwili wa mkewe huyo   na kuutupa pembezoni mwa nyumba ya jirani. “Alifika na watoto wao wawili na kimuita mkewe na kumtoa pembeni… sasa sisi tukadhani labda anaongea naye tu huko nyuma, kumbe huko ndiko alikomnyongea, ” alidai ndugu mmoja wa wanafamilia ya wanandoa hao.

Mashuhuda wengine walidai kuwa baadaye Msanjaa alikimbilia mlimani na kukamatwa siku iliyofuta asubuhi na wananchi hao waliokusanyana kwa kupiga yowe.

Wanadai mashuhuda hao kuwa wananchi hao walimkamata Masanja baada ya kumsaka na kushambulia kwa kipigo hadi kufa

Walidai kuwa Masanja alitengana na mkewe huyo baada ua kuchoshwa na vipigo vya mara kwa mara kila siku alipokuwa akirejea nyumbani akiwa amelewa. 
 
CHANZO: NIPASHE

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: