Agnes Gerald (Masogange)
Wasichana wawili raia wa Tanzania Agnes Gerald maarufu kama ‘Agnes
Masogange’ (25) na mdogo wake Melisa Edward (24) waliokamatwa zaidi ya
miezi 2 iliyopita katika uwanja wa ndege wa kimataifa Or Tambo, Afrika
Kusini wameachiwa kwa dhamana.
Melisa Edward

Mkuu wa Kitengo cha Dawa za Kulevya
Afrika Kusini, Kamishna Toto Mangaleni aliithibitishia MWANANCHI jana
kuwa watuhumiwa hao wameachiwa kwa dhamana, lakini wataendelea kubaki
Afrika Kusini wakati kesi yao ikiendelea.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Mangaleni
alisema wanawake hao ambao juzi pia walipanda kizimbani, walipata
dhamana hiyo jana kutoka Mahakama Kuu ya Gauteng iliyoko eneo la Kempton
Park jijini Johannesburg.
Hata hivyo, Kamishna Mangaleni alisema
hawezi kuzungumzia zaidi kuhusu kesi hiyo kwa sababu hataki kuharibu
uchunguzi ambao unaendelea dhidi ya Watanzania hao.
Marafiki wa karibu wa Masogange wanaoishi maeneo ya Midland Johannesburg ambao walikataa kunukuliwa majina yao, walithibitisha kuwa wanawake hao wameachiwa kwa dhamana.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Polisi cha Kuzuia na Kudhibiti Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa aliiambia Mwananchi jijini Dar es Salaam kuwa alikuwa amepata taarifa za kuachiwa kwa wasichana hao, lakini alikuwa anawasiliana na watu wa Afrika Kusini ili kupata uhakika.
Nzowa, hata hivyo alilidokeza gazeti hili juzi kuwa kuna uwezekano wanawake hao wangepata dhamana au kufungwa kifungo chepesi kwani dawa walizokamatwa nazo ni kemikali zinazotumika kutengeneza dawa za aina tofauti kwa matumizi ya binadamu ingawa pia na dawa za kulevya.
Ijumaa ya (July 5), shirika la habari la Afrika Kusini (SABC) liliripoti taarifa juu ya kukamatwa kwa wasichana wawili (ambao baadae walikuja kuthibitishwa kuwa ni Agnes Gerald na Melisa Edward) waliowasili na ndege kutoka Tanzania wakiwa wana mabegi sita makubwa ya dawa zinazoaminika kuwa ni `Crystal Methyl Amphetamine’ maarufu kama ‘Tik’ nchini humo, yenye thamani ya Rand 42.6 million sawa na zaidi ya billion 6 za Tanzania.
MWANANCHI




No comments:
Post a Comment