Fenesi ni miongoni mwa matunda ya msimu yenye umbo la kipekee
huku likiwa na ladha tamu isiyomithilika. Licha ya sifa hii, tunda hili
linatajwa kuwa na faida lukuki endapo litaliwa na mwanadamu.
Kwanza, linatajwa kuwa na virutubisho kadha wa
kadha vyenye kazi mbalimbali mwilini. Baadhi ya virutubisho hivyo ni
pamoja na vitamini za aina mbalimbali, madini, protini, mafuta, uwanga
na nyuzinyuzi.
Fenesi pia linatajwa kuwa chanzo kizuri cha
nishati kisichokuwa na lehemu. Si hivyo tu, bali pia ni chakula chenye
virutubisho vya kuondosha sumu mwilini vinavyoweza kuukinga mwili dhidi
ya saratani na magonjwa mengine kadha wa kadha.
Uwepo wa viondosha sumu ndani ya tunda hili
kunasaidia pia kuongeza uwezo wa kuona. Tunda hili pia linatajwa kuwa na
kiasi kikubwa cha madini ya potassium yanayosaidia kuimarisha mifupa
na afya ya ngozi.
Wataalamu wa mambo ya afya wamezitaja faida nyingine za tunda hili kuwa ni pamoja na:
Kinga: Fenesi ni chanzo kizuri
cha vitamini C. Uwepo wa kiasi kikubwa cha vitamini hiyo pamoja na
viondosha sumu kunaongeza ufanisi wa mfumo wa kinga mwilini. Husaidia
kuongeza kinga dhidi ya kifua, mafua na kikohozi.
Nishati: Ni tunda salama kiafya,
halina lehemu licha ya kuwa na kiasi kikubwa cha mafuta. Pia, lina
wanga na kalori kwa kiasi kikubwa. Sukari iliyomo ndani yake huchangia
kwa kiasi kikubwa kuimarisha mwili.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Hurekebisha msukumo wa damu na pia husaidia
kurahisisha mmeng’enyo wa chakula tumboni pamoja na kuukinga mwili
dhidi ya magonjwa ya moyo na kupooza.
Asthma: Inasadikika pia kuwa tunda hili lina uwezo wa kuukinga mwili dhidi ya ugonjwa wa pumu.
Si hivyo tu, fenesi lina vitamini muhimu katika utengenezaji wa damu mwilini.
*Maimuna Kubegeya kwa msaada wa mtandao
MWANANCHI
MWANANCHI




No comments:
Post a Comment