Mesut Ozil
Dirisha la usajili kwenye vilabu vya soka barani Ulaya jana lilifungwa rasmi. Hivi ndivyo mambo yalivyokwenda.
Klabu
ya Arsenal imemsaini Mesut Ozil kutoka Real Madrid kwa dau la rekodi
katika klabu hiyo, Paundi Milioni 42.5. Kiungo huyo amesaini Mkataba wa
miaka mitano kwa mshahara wa Paundi 140,000 kwa wiki Ozili anategemewa
kupewa jezi namba 11.
Marouane Fellaini akiwa na David Moyes
Klabu ya Manchester United imemsaini Marouane Fellaini kutoka Everton kwa paundi milioni 27.5.
Gareth Bale alipokuwa akitambulishwa kwa mashabiki wa Real Madrid
Klabu ya Real Madrid imekamilisha usajili wa Gareth Bale na jana
alitambulishwa kwa mashabiki wapatao 20,000 wameingia uwanjani kuangalia
utambulisho wa Bale wakati alipohamia kwa ada ya uhamisho wa dunia
£86million. Kwa usajili huo, Bale anakuwa mchezaji ghali zaidi katika
historia ya mchezo huo.
Endelea kusoma habari hii kwa kubofya hapa chini
Kaka alipo wasili Milan
Klabu ya AC Milan imemrejesha tena mchezaji wao wa zamani, Kaka kutoka
Real Madrid Kaka kwa mkataba wa miaka 2 Kaka amerudi AC Milan kwa
uhamisho huru.
Gareth Barry nae amejiunga na Everton akitokea Manchester City
Romelu Lukaku amejiunga na Everton kwa mkopo kutoka Chelsea
Peter Odemwingie’s amesajiliwa na Cardiff akitokea West Brom kwa dau la £2.5million
Source: Daily Mail
No comments:
Post a Comment