London, England. Kocha David Moyes ataiongoza Manchester United kuifuata Liverpool kwa mara ya kwanza leo kwenye Uwanja wa Anfield, huku Arsenal wakiwakaribisha Tottenham Spurs.
Moyes aliondoka Everton na kuchukua mikoba ya Sir
Alex Ferguson msimu huu, lakini sasa anarejea Merseyside ikiwa ni baada
ya michezo mitatu msimu huu.
Kikosi chake cha United kimekuwa na matokeo ya kuvutia wakishinda moja, sare dhidi ya Chelsea Jumatatu.
“Anfield ni sehemu ngumu wakati wote,” alisema
Moyes. “Ni uwanja mzuri nimejiandaa kurudi hapo, najua hali inavyokuwa
unapocheza kwenye uwanja ule ni wazi mechi itakuwa ngumu na ushindani
kama inavyokuwa wakati wote, ni matumaini yangu tutaondoka na pointi
tatu muhimu. Liverpool ni moja ya timu bora katika msimu huu.
“Kila mtu ananiambia kuhusu ushindani uliopo kati
ya Liverpool na United, ni kama ilivyokuwa kwa Everton. Nimejiandaa kwa
mchezo na nimekuja na Manchester United vyote vivyohusu mechi ya aina
hii najua.”
Liverpool inaingia kwenye mchezo huo wakiwa na
rekodi nzuri ya ushindi pamoja na kumkosa mshambuliaji wao aliyefungiwa
Luis Suarez.
Daniel Sturridge amechukua jukumu la ufungaji kwa
kufunga michezo yote miwili waliyocheza awali. Wakiwa na pointi sita
katika michezo miwili kunawafanya vijana wa Anfield kujiamini zaidi,
nahodha Steven Gerrard ni matumaini yake kasi yao ya ushindi
wataiendeleza leo.
“Kwa kipindi kirefu tofauti kati yetu na United,
Chelsea na sasa Manchester City imekuwa ni kubwa,” alikiri Gerrard.
“Kila mwaka tunajaribu kupunguza pengo hilo, nadhani msimu huu
tutarudisha heshima yetu
No comments:
Post a Comment